HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA

HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA
kiungo : HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA

soma pia


HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA


MANARA
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.
Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.
Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.
Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.
Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.
“Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema Tarimba.
Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.
“Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.
Kwa niaba ya TFF, Ofisa Habari wa Shirikisho, Alfred Lucas, wameyapokea mapendekezo hayo kutoka kwa Tarimba na kwamba tutafanyia kazi ili kurekebisha makosa hayo kwa manufaa ya soka la Tanzania.


Hivyo makala HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA

yaani makala yote HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/haji-manara-aachiwa-huru-jela-ya-soka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HAJI MANARA AACHIWA HURU JELA YA SOKA, KAMA NAMUONA VILE NA MANENO YA WAHENGA"

Post a Comment