CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji

CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji
kiungo : CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji

soma pia


CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji

Mwambawahabari

Na Neema Mathias
Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) kimeiomba Serikali kuondoa kodi kwa bajaji (pikipiki zenye magurudumu matatu) zinazotumiwa na watu wenye ulemavu kama miguu na pia kubeba abiria ili kujipatia kipato.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CHAWATA John Mlabu mapema leo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto na ajira kwa watu wenye ulemavu.

“Kupitia fursa ya kuondolewa kodi kwa vifaa vya watu wenye ulemavu tunaiomba Serikali izitambue bajaji kuwa ni moja ya nyenzo inayomsaidia mtu mwenye ulemavu na hivyo ziondolewe kodi, na Serikali iziagize kwa wingi na kuzikabidhi kwa watu wenye ulemavu kwa mkopo kupitia Umoja wa Waendesha Bajaji Dar es Salaam (UWAWABADA),” amesema Mlabu.
Ameendelea kwa kusema, kupitia UWAWABADA bajaji hizo zitatawanywa kote nchini kwa utaratibu walionao ili ziwainue kiuchumi na kuboresha maisha yao na familia zao.
Aidha Mlabu amesema, CHAWATA kinamuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kuangalia kundi hilo kupitia mafanikio ya watu wenye ulemavu Jijini, Dar es Salaam na kurasimisha shughuli ya uendeshaji wa bajaji kuwa ya watu wenye ulemavu pekee na wengine wasio na ulemavu waendeshe pikipiki za kawaida (Bodaboda).
“Kuendesha Bajaji ni ajira pekee ambayo haina usumbufu kwetu na imeyagusa makundi yote ya wanawake na wanaume tena rika zote, maana kwenye ujenzi wa viwanda na makampuni sisi hatuajiriwi, licha ya uwepo wa sheria Na. 9 ya 2010 ya ajira kwa walemavu inayotaka kila mahali pa kazi 3% ya watumishi wake wawe watu wenye ulemavu,” amefafanua Mlabu.
Vile vile amesema, uwepo wa chombo hicho cha magurudumu matatu kimewasaidia sana walemavu kujipatia kipato na kuwaondoa katika maisha ya kuombaomba kama ilivyokuwa hapo awali, aidha amesema kuwa wanaichangia Serikali katika kukuza uchumi wa nchi kupita kodi mbalimbali za Serikali pale wanaponunua mafuta ama vipuli vya bajaji zao.
CHAWATA kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano na Rais Dkt. Magufuli kwa kujali watu wa tabaka la chini na maskini katika Taifa hili, ambapo wameshuhudia mara nyingi katika ziara zake akiwatetea wafanyabiashara wadogo (Machinga), Wakulima na Wafugaji, hivyo wanamuona Rais Magufuli kuwa ni Rais wa wanyonge.


Hivyo makala CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji

yaani makala yote CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/chawata-chaiomba-serikali-kuwaondolea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CHAWATA Chaiomba Serikali Kuwaondolea Kodi ya Bajaji"

Post a Comment