title : CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE.
kiungo : CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE.
CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE.
Mwambawahabari
Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimemuomba Rais Dkt. John Magufuli katika miaka mitatu iliyobaki kubadilisha msimamo wa kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara nchini itakayo fanywa na vyama vya upinzani.
Hayo yamesemwa mapema leo hii jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Doyo amesema wao wanania nzuri ya kufanya siasa tofauti na vyama vingine nakusema Rais asione kwamba vyama vyote vya upinzani vinakauli mbovu katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
"shughuli za siasa ni haki ya kila chama kikatiba kwani kuzuia shughuli hizo ni kubinya uhuru na taratibu zilizoelekezwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema
Aidha, Chama hicvho kitaadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake kwa kufanya ziara ya kutembea vyombo vya habari mbalimbali ili kuweza kutoa ushirikiano na kujitangaza hasa katika kuelezea mafanikio yao waliyoyapata.
Pia Doyo amesema Chama hicho kitafanya maadhimisho hayo kwa njia ya ziara ambapo watatembelea baadhi ya taasisi za kidini, magereza pamoja na hospitali kwa kuchangia kutoa damu.
Ziara ya chama hicho imeanza leo hii katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda lakini hawakupata fursa ya kukutana na mkuu mkoa huyo kutokana na kuwa nje ya ofisi.
Hivyo makala CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE.
yaani makala yote CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/chama-cha-adc-chamuomba-rais-magufuli.html
0 Response to "CHAMA CHA ADC CHAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUBADILI MSIMAMO WAKE."
Post a Comment