title : SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI
kiungo : SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI
Benny Mwaipaja, WFM
Serikali imesema inaendelea kupitia sheria, kanuni na taratibu za misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa misamaha yote isiyokuwa na tija inafutwa na hivyo kuiwezesha Serikali kuongeza mapato kwa ajili ya kupeleka huduma za maendeleo kwa wananchi wake.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Masasi, Mhe. Rashid Mohamed Chuachua (CCM), aliyetaka kujua namna Serikali inavyodhibiti misamaha ya kodi tangu irekodiwe kwa viwango vya juu Mwaka wa Fedha 2011/2012.
Mhe. Chuwachuwa alihoji mwenendo wa utoaji wa misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa maelezo kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizopoteza fedha nyingi kwa ajili ya misamaha ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kigezo cha kuvutia Wawekezaji.
Alisema kuwa kwa mujibu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2009-2010, Tanzania ilipoteza asilimia 15 ya Pato la Taifa lililotarajiwa kukusanywa kutokana na misamaha ya kodi, mwaka 2010-2011 asilimia 8, kwa mwaka 2011-2012 asilimia 27 ya mapato ya Serikali yalipotea.
“Je hali ya misamaha ya kodi kuanzia 2013-2014 hadi sasa ikoje’’. Alihoji Mhe. Chuachua.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),misamaha ya kodi kama sehemu ya asilimia ya Pato la Taifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi sasa imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka.
Hivyo makala SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI
yaani makala yote SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/serikali-yaahidi-kuendelea-kupitia-upya.html
0 Response to "SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI"
Post a Comment