title : PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR
kiungo : PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR
PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU wa NEC, Idara ya Organazesheni ya CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima amewataka viongozi na watendaji wanaochaguliwa kwenye uchaguzi wa chama na jumuiya zake kwa sasa kuwa na fikra na mitizamo mipya itakayoongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya CCM.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za siasa za Mikoa ya CCM Mjini na Magharibi pamoja na wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko Amani Unguja, alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara kutokana na utamaduni wa kupata viongozi kwa njia za kidemokrasia hasa Uchaguzi huru na wa haki.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama sambamba na kujitambulisha kwa viongozi hao kwani tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni Mjini Dodoma hiyo ndio ziara yake ya mwanzo.
Alizitaka kamati mbali mbali zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuchuja viongozi katika uchaguzi wa chama hicho kuhakikisha wanapatikana viongozi wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji ndani ya chama hicho na sio wababaishaji.
Ni Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho wakimsikiliza kwa Umakini Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima huko Katika Ukumbi wa CCM Amani Unguja.
Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa,Nd. Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko Katika Ukumbi wa CCM Amani Unguja.
Hivyo makala PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR
yaani makala yote PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/pereira-atoa-nasaha-nzito-kwa-viongozi.html
0 Response to "PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR"
Post a Comment