title : BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI
kiungo : BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI
BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI
Watu wawili waliokuwa wakidai kuwa ni Askari wa Ssalama barabarani wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na madereva pikipiki wakati wakijaribu kutekeleza jukumu la ukamataji wa pikipiki zisizo na leseni.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Katunguru kata ya Katunguru wilayani Sengerema wakati watu hao ambao hawakuweza kujulikana majina yao walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao, baada ya kuanza kukamata pikipiki pasipo kuwa na vitambulisho vya kazi pamoja na kutovaa sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Wameongeza kuwa baada ya kuwashambulia watu hao kwa kuwadhania kuwa wezi wa pikipiki, walikili kuwa wao sio maaskari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wala hawahusiani na jeshi la polis lakini walikuwa wakitumiwa na Jeshi la Polisi kituo cha katunguru kukamata pikipiki.
Madereva hao waliliomba Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kuhakikisha shughuli za ukamataji wa pikipiki zina simamiwa na maaskari wenye weledi wa kazi hiyo ilikuepuka mataperi wa pikipiki ambao wamekuwa wakitumia nafasi ya Jeshi la Polisi kuiba pikipiki hususani kwa madereva pikipiki.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alipohojiwa alisema Ofisi yake haija pokea taarifa za tukio hilo na kuahidi kufuatilia tukio hilo.
Hivyo makala BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI
yaani makala yote BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/bodaboda-mwanza-wawapa-kichapo-askari.html
0 Response to "BODABODA MWANZA WAWAPA KICHAPO ASKARI FEKI WA USALAMA BARABARANI"
Post a Comment