WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI
kiungo : WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI

soma pia


WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND NCHINI 11-13 APRILI 2018

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland, Mhe. Prof. Jacek Craputowicz atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 hadi 13 Aprili 2018. Katika ziara hiyo, Prof. Craputowicz pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) Jijini Dar Es Salaam tarehe 12 Aprili 2018. Viongozi hao watajadili namna ya kuboresha mahusiano na mashirikiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Poland, hususan katika eneo la uwekezaji na biashara. 

Poland ni moja ya nchi zinazounga mkono Sera ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020. Katika kuunga mkono Sera hiyo, Serikali ya Poland imetoa mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 110 kwa Serikali ya Tanzania. 

Kati ya fedha hizo, Dola za Marekani milioni 55 zimetumika kujenga kiwanda cha kuunganisha matrekta Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani ambacho kimeshaanza kazi na Dola za Marekani milioni 55 ni kwa ajili ya kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya kilimo katika mikoa minane ya Rukwa, Katavi, Manyara, Ruvuma, Dodoma, Shinyanga, Njombe na Songwe.

Prof. Craputowicz na mwenyeji wake watashiriki hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa ofisi ya Ubalozi wa nchi hiyo zilizopo nyumba namba 15, mtaa wa Mtwara, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Aprili 2018. Poland ilifungua upya Ubalozi wake nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya. 

Baada ya ufunguzi viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi hizo saa tano asubuhi. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam
10 Aprili, 2018


Hivyo makala WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI

yaani makala yote WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/waziri-wa-mambo-ya-nje-wa-poland-kuzuru.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI"

Post a Comment