BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
kiungo : BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

soma pia


BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini.

Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha chombo hicho kinachoongoza mapambano ya dawa za kulevya ili kiendelee kufanya kazi kwa weledi na kwa kutumia mbinu za kisayansi.

“Tunaponadi uchumi wa viwanda lazima tuwe na nguvu kazi yenye siha njema kuweza kushiriki kwenye kazi halali za kujenga Taifa letu na yeyote anayetaka kudhohofisha nguvu kazi ya Taifa letu au kuhujumu jitihada za uchumi wa viwanda atashughulikiwa bila huruma,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017.
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawa mbalimbali za kulevya katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga .



Hivyo makala BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

yaani makala yote BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/biashara-ya-dawa-za-kulevya-kuwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA"

Post a Comment