title : Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima
kiungo : Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima
Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima
Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kuepuka ajali zisizo za
lazima kwani tangu mwaka 2008 hadi Mei 2017 zimetokea ajali 125 kwenye
migodi yenye leseni na vifo ni 213.
Ajali zilizotokea kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wasio na leseni
nchini (maeneo ya mifumuko ya uchimbaji madini) katika kipindi hicho
ni 56 na kusababisha vifo vya wachimbaji 140.
Kamishna wa madini nchini, mhandisi Benjamin Mchwampaka aliyasema hayo wakati akizungumza na mameneja na wamiliki wa migodi mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Mhandisi Mchwampaka alisema ajali nyingi kwenye migodi ya wachimbaji
wadogo zinasababishwa na uzembe, kwani kwa mwaka huu pekee hadi Mei 15 ajali zilizotokea ni 11 na kusababisha vifo 26.
Alisema kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani,
ajali zilizotokea kwa wachimbaji wadogo kwa kipindi cha 2008/2017 ni
31 na wachimbaji wadogo waliopoteza maisha ni 40.
Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenyemafunzo ya usalama migodini.
Kamishna wa madini Tanzania, mhandisi Benjamin Mchwampaka akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kuhusiana na usalama kwenye migodi yao.
Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenye
mafunzo ya usalama migodini.
Hivyo makala Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima
yaani makala yote Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/wachimbaji-wadogo-wa-madini-nchini.html
0 Response to "Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima"
Post a Comment