SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.

SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.
kiungo : SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.

soma pia


SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.

Mwambawahabari
0151-Mhe.Mwinyi
Na Husna Saidi & Nuru Juma
Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa inampango wakuunda kikosi kazi cha kupitia changamoto zinazowakabili Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Sita kutojiunga na mafunzo yaJeshi kama sheria ya Jeshi la kujengaTaifa inavyotaka.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Hussein Mwinyi alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na George Huruma Mkuchika Mbunge wa jimbo la Newala Mjini.

Dkt. Mwinyi alisema kuwa Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 1964 imeweka ulazima wa vijana wa Tanzania wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria, hatahivyo mwaka 1994 Serikali iliyasitisha kwa muda mafunzo hayo na kuyarejesha tena mwaka 2013 na yanaendelea hadi sasa.
“Takwimu zilizopo zinaonyesha kupungua kwa idadi ya vijana wanaojiunga na mafunzo hayo muhimu ya jeshi la kujenga Taifa hali hii imesababishwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugongana kwa tarehe za kuanza mafunzo ya vijana kwa mujibu wa sheria na kufunguliwa kwa vyuo mbalimbali hapa nchini ambapo mihula ya mafunzo huanza”, alisema Dkt. Mwinyi.
Aidha alisema hali hiyo imewafanya vijana wengi walioteuliwa kujiunga na vyuo kukosa nafasi ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwamujibu wa sheria na changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu, rasilimali watu na pamoja na fedha, hatahivyo Serikali inaendelea na juhudi za kupata suluhu ya changamoto hizo.
Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa mwaka 2014 vijana waliohitimu kidato cha sita walikuwa 41,968 na kati yao waliojiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa walikuwa 31,692 ambao ni sawa na asilimia 75.5.
Aidha mwaka 2015 kulikuwa na wahitimu 40,753 na waliojiunga ni 19,990 sawa na asilimia 48.8 huku mwaka 2016 wahitimu kidato cha sita walikuwa 63,623 waliojiunga na Jeshi ni 14,747 sawa na asilimia 23.2.
Zoezi la kuwachagua vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa halina vigezo maalum kwani kila kijana aliyemaliza kidato cha sita anasifa ya kujiunga na mafunzo hayo.



Hivyo makala SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI.

yaani makala yote SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-kutafuta-ufumbuzi-kuhusu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUTAFUTA UFUMBUZI KUHUSU WANAFUNZI KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JESHI."

Post a Comment