SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI
kiungo : SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

soma pia


SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

Mwambawahabari
PMO_6318
Na Nuru Juma & Husna Saidi
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaendelea na kutekeleza  miradi mbalimbali ya maji Mijini na Vijijini ili kuhakikisha Taifa linaondokana na kero itokanayo na maji.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge alipokuwa akijibu swali la Mhe, Leah Jeremiah Komanya Mbunge wa viti Maalum.

Mhandisi Lwenge alisema katika kuhakikisha miradi hiyo inanufaisha jamii kama ilivyokusudiwa Wizara yake imeandaa na inatekeleza uundaji, usajili wa vyombo vya watumiaji maji (COWSOs) na kuzijengea uwezo kwaajili ya uendeshaji na usimamizi.
“Pamoja na utekelezaji huo kumekuwa na changamoto mbalimbali katika miradi hiyo ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya maji, wizi wa vifaa vya maji pamoja na watumiaji maji kutolipa huduma hiyo zikiwemo taasisi za Serikali hali hiyo imepelekea mamlaka nyingi kushindwa kugharamia matengenezo ya miundombinu ya maji” alisema Mhandisi Lwenge.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na wizi wa maji pamoja na uchakavu wa miundombinu Wizara inaendelea kurekebisha Sheria za maji ili ziweze kutoa adhabu kali kwa wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji.
Aidha alisema kuwa katika kuhakikisha mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira zinatoa huduma endelevu mamlaka hizo zinasimamiwa na bodi ambazo zinajumuisha wadau mbalimbali.
Kwa upande mwingine alisema mamlaka za maji  safi na usafi wa mazingira mijini zinaendelea kukarabati miundombinu ya maji iliyochakaa, kufunga dira za maji kwa wateja wote ili kubaini matumizi yao halisi na kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya maji.
Aidha Wizara imeanza kuchukua hatua za kutumia nishati ya jua kwenye mitambo ya maji hususani vijijini kwaajili ya kupunguza gharama za uendeshaji.


Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-kuendelea-kutekeleza-miradi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI"

Post a Comment