title : Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu
kiungo : Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu
Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu
Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.
Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi232,974,660,” alisema.
Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.
“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.
“Kama sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa nchi kwani wanamichezo wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua yote haya yanawezekana na dalili zimeanza kuonekana.
Alisema Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo mingine kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika kutangaza Taifa na pia michezo huchangia kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.
“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau timu zote zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa zawadi zao leo.
Ni matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza kuandaliwa vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,” alisema Hisham.
Hivyo makala Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu
yaani makala yote Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/vodacom-yaongeza-bajeti-ya-zawadi-ligi.html
0 Response to "Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu"
Post a Comment