title : AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR
kiungo : AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR
AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR
Kambi ya watoto na vijana inayosimamiwa na Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) maarufu kama Ariel Camp 2018’ iliyoshirikisha washiriki 50 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu imefungwa leo Ijumaa Disemba 14,2018 jijini Dar es salaam.
Akifunga kambi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS), Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume hiyo Bw. Jumanne Issango aliipongeza AGPAHI kwa kuanzisha kambi hizo zinazolenga kuwapa watoto na vijana msaada wa kisaikolojia utakaowawezesha kukabialiana na changamoto zinazowakabili.
“Naishukuru AGPAHI kwa kutoa msaada huu wa kisaikolojia kwa watoto na vijana kwani huduma hiyo ni muhimu sana kwa afya na ustawi wao hasa ikizingatiwa kuwa changamoto hizo zinawaathiri kimwili, kiafya, kijamii na kisaikolojia,” alisema Bw. Issango.
Aidha aliitaka jamii kubadilika na kuacha vitendo vya kunyanyapaa wanaoishi na maambukizi ya VVU huku akiwahamasisha watoto na vijana hao kutumia kwa usahihi dawa za kufubaza makali ya VVU ili kuimarisha afya zao.
“Ili kuishi maisha bora na kukamilisha ndoto zenu za baadaye nawakumbusha kuwa ARV ndiyo mpango mzima, Watu wasiotumia vizuri dawa hizi afya zao zimekuwa zikitetereka na kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na hata kufa. Kamwe msiache kutumia dawa kwa sababu yoyote ile,” alisisitiza.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akizungumza katika ukumbi wa Serene Beach Resort wakati akifunga Ariel Camp 2018 kwa niaba ya Mkurugenzi wa TACAIDS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili,kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu.
Washiriki wa Ariel Camp wakimsikiliza mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI wakati wa kufunga Ariel Camp 2018.
Waliokaa ni washindi wa shindano la Mr & Miss AGPAHI Ariel Camp wakiwa katika picha ya pamoja na jaji Lugano Maclean (wa kwanza kulia) na kiongozi wa washiriki wa shindano la Urembo 'Mr & Miss Ariel Camp' Agnes William ( wa kwanza kushoto) na washiriki wa shindano hilo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR
yaani makala yote AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/agpahi-ariel-camp-2018-yafungwa-dar.html
0 Response to "AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR"
Post a Comment