title : Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha
kiungo : Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha
Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha
BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.
Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo.
Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo.
Akizungumza leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.
Alisema droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha
yaani makala yote Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/biko-kutoa-milioni-20-jumatano-hii.html
0 Response to "Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha"
Post a Comment