title : Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
kiungo : Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
Timu ya Michezo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa lengo la kudumisha uhusiano na ushirikiano kati ya hospitali hizi.
Ushirikiano huu unadumisha utamuduni wa hospitali hizi kutembeleana kila mwaka na kushiriki michezo ya Pasaka ambayo imeanza leo Kisiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt.Juma Mbwana amesema ushirikiano baina ya hospitali hizi ni mzuri na pia wamefurahi kujumuika pamoja katika kufanya usafi.
Mkurugenzi huyo amesema na kuahidi shughuli ya usafi itakuwa ikifanyika mara kwa mara ili kudumisha uhusiano zaidi.
“Serikali ya Mapunduzi Zanzibar chini ya Rais Dkt. Mohamed Shein na Wizara ya Afya tumefurahiswa na ugeni huu kwani michezo ni afya, pia kuja kwenu hapa hospitalini kufanya usafi kumewafariji na kuhamasisha wananchi kufanya usafi,” amesema Dkt. Mbwana.
Kwa upande wake Mkuu wa msafara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo amesema katika sekta ya afya michezo na usafi ni vitu muhimu na kwamba lazima mambo haya yatekelezwe.
Pia, ametoa wito kwa jamii kushiriki kwa hiari kutoa huduma za usafi hospitalini.
“sisi tumetokea kwenye sekta ya afya tumeona ni vizuri tutumie fursa hii kujumuika na wenzetu katika sekta ya afya katika michezo, lakini tumeona tuje tufanye usafi hospitali kwa kuwa usafi ni muhimu kwenye sekta ya afya,” amesema Dkt. Praxeda.
Michezo hii ya Pasaka hufanyika kila mwaka zikihirikisha timu ya Muhimbili na Wizara ya Afya Zanzibar.
Mkurugenzi wa idara ya tiba kutoka wizara ya afya Zanzibar Dkt. Juma S. Mbwana, akizungumza jambo kwa wanamichezo wakati wa zoezi la usafi ambapo wameshiriki katika kufanya maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa huduma za tiba shirikishi kutoka Hospitali yaTaifa Muhimbili Dkt. Praxeda Ogwayo (kulia) akishiriki kufanya usafi katika moja ya wodi hospitali hapo, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa huduma za uuguzi na ukunga Bw. Yassin Mungwatosha kutoka muhimbili.
Baadhi ya wanamichezo wa Muhimbili wakishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Wanamichezo wa Muhimbili wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi.
Hivyo makala Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
yaani makala yote Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/muhimbili-yafanya-usafi-hospitali-ya.html
0 Response to "Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar"
Post a Comment