Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa

Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa
kiungo : Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa

soma pia


Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa

Na MbarakaKambona,

Wadau wa haki za binadamu kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za serikali, taasisi binafsi na wafanyabiashara wamekuta na kupitia rasimu ya kwanza ya mapendekezo ya Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara.

Wadau hao walikutana Agosti 23, 2017 katika kikao kilichofanyika katika ofisi zaTume ya Haki za Binadamu jijini Dar es Salaam kujadili rasimu hiyo kufuatia utafiti uliofanywa na wataalamu na maoni yaliyokusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali ya biashara.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri alisema kuwa kuanzishwa kwa mpango huo kumelenga katika kuhakikisha kuwa mifumo yote ya kitaifa na kimataifa ya sera na sheria inazingatia na ulinzi na utetezi haki za binadamu wakati wote wa utekelezaji wa majukumu ya kibiashara na kuweka mifumo ya utatuzi wa migogoro ya waathirika pale itakapojitokeza.

Utafiti huo ambao ulifanyika Mei, 2017 ulihusisha wadau mbalimbali wakiongozwa na Tume, zikiwemo taasisi za serikali, taasisi binafsi, wafanyabiashara na wananchi ulifanyika katika maeneo maalum yaliyochaguliwa ikiwemo maeneo ya kilimo katika Mkoa wa Mbeya- Mbarali, Maeneo ya viwanda Mkoani Dodoma na Singida na maeneo yaUtalii upande wa Zanzibar uliofanyika.

Utafiti huo unafuatia tamko la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilitolewa mwaka 2011 linalotaka nchi wanachama kuanzisha Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika maeneo ya biashara ili kutoa muongozo wa kulinda uvunjifu wa haki za binadamu katika maeneo hayo.

 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri akiongea na washiriki wa kikao cha wadau wa haki za binadamu wakati akifungua mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Tume zilizopo  jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2017. Kulia kwake ni Kamishna Mkaazi wa Tume Zanzibar, Mhe. Mohamed Hassan na Kushoto kwake ni  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Bwn. Francis Nzuki
 Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Bwn. Francis Nzuki akiongea katika kikao cha wadau wa haki za binadamu mara baada ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Iddi Ramadhani Mapuri (katikati) kufungua rasmi mkutano huo.
 Mmoja wa watoa mada ya haki za binadamu na biashara, Bi. Nora Gotzmann akiwasilisha mada yake iliyohusu masuala ya Biashara na Haki za Binadamu, jinsi ya kulinda, kuheshimu na namna ya kupata utatuzi wa migogoro inapojitokeza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa

yaani makala yote Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/mpangokazi-wa-kitaifa-wa-haki-za.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mpangokazi wa kitaifa wa Haki za Binadamu katika biashara mbioni kukamilishwa"

Post a Comment