title : MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.
kiungo : MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.
MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.
Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili saa 6:00 usiku huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Hivi sasa Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura ambapo anaendelea kufanyiwa vipimo vya awali na kisha atalazwa ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu Zaidi siku ya Alhamisi.
“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda Hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu. Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni” hayo ni maelezo aliyotoa Mariam kupitia picha ya video iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii.
Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB) aliuagiza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kumtafuta Mariam ili apelekwe Hospitalini hapa kwa ajili uchunguzi na matibabu.
Mariam ameletwa na gari la wagonjwa (ambulance) kutoka Singida lililoanza safari yake saa 8:00 mchana jana. Tutaendelea kuwapa taarifa juu ya mwenendo wa matibabu yake.
Hivyo makala MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.
yaani makala yote MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/mgonjwa-mariam-rajab-wa-singida-awasili.html
0 Response to "MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU."
Post a Comment