WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA
kiungo : WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

soma pia


WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Bukoba Mkoani Kagera leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nane kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Januari 2, 2019 mjini Bukoba kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika uwanja wa uhuru mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zinazowakabili. 

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru eneo la Mayunga hapa mjini Bukoba, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huu wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola. 

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea. 



Hivyo makala WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-lugola-kuanza-ziara-ndefu-mkoani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA"

Post a Comment