KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO

KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO
kiungo : KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO

soma pia


KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO

KAMPENI za Uchaguzi Mkuu wa Yanga zimezinduliwa rasmi leo kwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa uzoefu wake katika sekta ya michezo utamsaidia kuibadilisha Yanga na kuleta mabadiliko.

Dkt. Msolla amezindua kampeni hizo katika makao makuu ya Klabu ya Yanga na kunadi sera zake mbele ya wanachama wa klabu hiyo na kueleza kuwa uzoefu wake katika sekta ya  michezo kwa muda wa miaka 40 utamsaidia kuweza kutekeleza mipango ya klabu kwa wakati na lengo kuu ni kuirudisha timu kwa Wananchi.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, Msolla amesema kuwa amedhamiria kuleta mabadiliko ndani ya Yanga ili kutatua changamoto zilizopo kwenye taasisi hiyo ikiwemo ya uongozi ambalo lilikuwa linaathiri ufanisi wa klabu.

"Kwa kipindi kirefu kumekuwa na changamoto ya kiuongozi na matokeo yake changamoto hiyo imefanya kuwe na ombwe la uongozi, nimeamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu kwa sababu nina uzoefu wa kutosha hasa baada ya kuwa kwenye tasnia ya mpira kwa muda wa miaka 40 katika nyanja mbalimbali,"

"Nitahakikisha ninajenga umoja ndani ya klabu kwa wanachama na wapenzi wa Yanga na kuirudisha timu kwa wananchi kwa kuimarisha matawi yaliyopo, kuanzisha matawi mapya, matawi kupelekewa katiba ili wawe na uelewa wa katiba ya klabu yao na kuendeleza mchakato wa maboresho ya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

"Nitahakikisha Yanga inatengeneza Historia yake kwa kuboresha eneo la klabu na kufanya iwe sehemu ya utalii kama ulaya bila kusahau maboresho ya uwanja wa Kaunda pamoja na ukarabati wa jengo la klabu pamoja na kuweka misingi bora ya uwajibikaji," amesema Msolla na kuomba wanachama wamchague.

Yanga inatarajia kufanya uchaguzi wake Mei 5 mwaka huu na leo kampeni zimezinduliwa rasmi kwa wagombea ili kupata viongozi wapya kwa ngazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga.


Hivyo makala KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO

yaani makala yote KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/kampeni-za-uchaguzi-wa-yanga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO"

Post a Comment