WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO

WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO
kiungo : WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO

soma pia


WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WANANCHI wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wameswa  na serilali  kuvilinda na kuvitunza kwa kuacha kufanya shughuli za kijamii. kwenye maeneo hayo.


Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo wakati wa ziara yake katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu.Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Kalobelo amesema wananchi wanatakiwa kuvitunza vyanzo vya maji ili maji yaendelee kuwepo kwa matumizi ya kila siku.

Amesema, chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni mto Ruvu, kukiwa na Ruvu juu na Ruvu chini na wananchi wanazidi kuongezeka karibia na mto huo."Wananchi wanazidi kuongezeka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruvu ambao ndio chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na katikka sheria za mazingira inawataka wananchi wakae mita 60 kutoka kwenye mto,"amesema Mhandisi Kalobelo.

Ameeleza kuwa, wananchi wanaoishi kando ya maeneo hayo wanatakiwa kuacha kupanda miti inayonyonya maji au kutumia maji mengi bali wanatakiwa kupanda miti inayovutia maji kuwepo kwenye  vyanzo hivyo.

Mbali na hilo, Mhandisi amesema shughuli za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji vinaweza kusababisha kuharibu vyanzo vya maji na kusababisha kukosekana kwa maji ambapo kwa sasa maji yapo kwenye wastani unaowatosheleza wananchi wa Dar es Salaam kwa asilimia kubwa.

Aidha, katika ziara hito, Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi wa Usafu na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.Mhandisi Kalobelo ametemebelea maeneo mbalimbali ya miradi ya ujenzi wa matenki na upanuzi wa mtambo utakaofanikisha kupatikana kwa maji kwenye maeneo yalioyokuwa hayapo kwenye mtandao hapo awali.

Amewapongeza DAWASA  kwa jitihada wanazozionyesha kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji na ametoa rai kwa wananchi wajiunge kwenye mradi huu ili wapate maji safi na salama.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa ameambata na Mkurugenzi wa Usafi na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili kulia)  wakati alipotembelea Chanzo cha uzalishaji maji cha Ruvu Juu katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya DAWASA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanule Kalobelo  akielezea jambo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  na Mkurugenzi wa Usafi na Mazingira wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Mjumbe wa bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba.


Hivyo makala WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO

yaani makala yote WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wananchi-wanaoishi-kando-ya-mito-waache.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANANCHI WANAOISHI KANDO YA MITO WAACHE KUHARIBU VYANZO VYA MAJI- MHANDISI KALOBELO"

Post a Comment