title : RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI
kiungo : RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI
RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kitendo cha timu za Taifa kufungwa anatamani siku moja awe Waziri wa Michezo ili apange timu mwenyewe.
Magufuli amesema huwa anaumia sana na ameboreka kwa kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys kufungwa mabao mengi katika ardhi ya nyumbani.
Akizungumza leo wakati wa hotuba mbele ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wilayani Kyela, Magufuli amesema hajafurahishwa na timu ya vijana kufungwa mabao mengi tena wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani na mashindano wakiwa wameandaa wenyewe.
"Hii ni aibu kwa Taifa, tupo milioni 55 tukifungwa tunaaibika wote haiwezekani Waziri unaangalia tu labda kufungwa ni mchezo mzuri, mashindano tumeaandaa wenyewe, uwanja wa kwetu wenyewe, tumefungwa mabao mengi kwelikweli, hili ni jambo la ajabu ungechukua hata timu ya Kyela tusingefungwa hivi, " amesema Magufuli.
"Sasa hili linapaswa liangaliwe kwa usawa, ninatamani siku moja niwe Waziri wa Michezo na nikiwa Waziri wa Michezo timu nitaipanga mwenyewe, na timu nyingine hiyo nayo inajiandaa sijui na wao watapigwa kama hawa,"
Michuano ya Afcon ambayo imemalizika wikiendi hii, Cameroon imebebwa ubingwa kwa vijana, huku Tanzania ikitolewa na zigo la mabao 12 ya kufungwa na imefunga mabao sita pekee kwenye michezo mitatu.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI
yaani makala yote RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/rais-magufuli-asikitishwa-kufanya.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI"
Post a Comment