title : TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU
kiungo : TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU
TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU

Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima akiwaonyesha moja ya taarfa ya utekelezaji majukumu kwa Timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT),(hawapo pichani) katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Mwonekano wa kwa Timu za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT)wakiwa katika katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Baadhi ya wajumbe katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI wakimsikiliza kwa umakiniDkt.Gwajima .
…………………………………..
Na. Majid Abdulkarim
Kamati za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya(CHMT) nchini zimetakiwa kuwa wabunifu katika kutekeleza shughuli zake na kuhakikisha wanaboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa kwa ujumla ili kuleta matokeo bora kwa watanzania.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima katika kikao cha Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Dkt. Gwajima amesema kuwa ubunifu unaotakiwa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya mteja na mtoa huduma za afya ili mteja awezekuwa uhuru na kujisikia faraja katika kupata huduma kutoka kituoni hapo.
“Mahusiano mazuri yanajengwa na ukarimu, lugha nzuri kwa mteja na utendaji kazi wenu kwa ujumla mnavyo hudumia wateja wenu kwa kuwa mawakili wazuri katika jamii yao kulingana na mlivyo wahudumia” Ameseama Dkt.Gwajima
Lakini pia Dkt.Gwajima amewataka watoa huduma za afya kuwa na mpango kazi utakao weza kuwaongoza vyema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kufikia kiwango bora cha utoaji huduma za afya nchini.
Dkt.Gwajima ameeleza kuwa mpango kazi kwa mtumishi utasaidia kuweza kupata tathimini ya utekelezaji wa amjukumu ya mtoa huduma za afya na kujua matokeo yapi yamefanyikiwa , kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia suluhisho ili kufikia malengo ya mtoa huduma aliyojiwekea katika mpango kazi wake.
“Ili kupata tathimini ya utendaji kazi wa watoa huduma za afya amesisitiza kuhakikisha kila mmoja kuwa na taarfa ya uwajibikaji wake ukiwa na takwimu sahihi ili kuweza kupata matokeo bora katika sekta ya faya”.Ameongezea Dkt.Gwajima
Aidha Dkt.Gwajima amehitimisha kwa kuwataka watoa huduma za afya kutekeleza mipango kazi yao kwa vitendo ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayo onyesha mabadili katika sekta ya afya na hapo tutakuwa tumetimiza azma ya serikali ya kumuhudumia mwananchi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Samwel Seseja amesema kuwa atasimamia vyema maelekezo yalotolewa na Dkt.Gwajima ili kuhakikisha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa zina boreka na kuimarishwa vizuri kwa faida ya watanzania.
Hivyo makala TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU
yaani makala yote TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/timu-za-uendeshaji-wa-huduma-za-afya.html
0 Response to "TIMU ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA NA WILAYA ZATAKIWA KUWA WABUNIFU"
Post a Comment