title : WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI
kiungo : WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI
WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI
Na Woinde Shizza ,Globu ya jamii Arusha
WANAFUNZI ambao wamemaliza masomo elimu ya darasa la saba mwaka 2018 na kufanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari wanaoishi Kata ya Odonyowasi katika Halmashauri ya Arusha, wameepukana na adha ya kutembea umbali mrefu baada ya Serikali kuwapangia Sekondari ya Oldonyowasi ambayo ni
mpya na ipo ndani ya kata hiyo.
Kabla ya kukamilika kwa sekondari hiyo wanafunzi wanaosoma masomo ya sekondari kutoka ndani ya kata hiyo walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 16 kwenda na kurudi shuleni katika Shule ya Sekondari ya Oldonyosambu.Umbali huo ulikuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi ikiwemo ya wengi wao kutofanya vizuri kwenye masomo na wengine kuacha shule.

Hivyo wazazi, walezi na wananchi wa Kata hiyo waliweka mkakati kuhakikisha wanaondoa changamoto hiyo ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.Waliamua kuchangishana fedha pamoja na kuomba msaada wa wadau wa maendeleo wakiwamo TANAPA na Serikali kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumza leo Januari 30, 2019, Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyowas Geophray Ayoa amesema ujenzi wa sekondari hiyo mpya ya Oldonyowas, ulianza mwaka 2018 baada ya wazazi kukerwa na changamoto zinazowakabili watoto wao, hasa ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata elimu ya sekondari. "Ujenzi ulianza kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na TANAPA kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu na vyoo pamoja na samani za ofisi na za madarasa kwa gharama ya Sh.milioni 70 huku TANAPA wakitoa Sh.milioni 50 na wananchi Sh.milioni 15,"amesema.
Aidha ameipongeza Serikali kupitia mradi wa TASAF awamu ya III, kwa kuunga mkono juhudi za wananchi wa Oldonyowas, kwa kuongezea nguvu na kufanikiwa kujenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi ndogo ya walimu, nyumba ya walimu yenye sehemu mbili (2 in 1), vyoo na jengo la utwala pamoja
na kununua samani za ofisi na madarasa.Jumla ya Sh.milioni 229.4 zimetumika."Tayari imeanza kupokea wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza."
Pia amesema wananchi wa Oldonyowas wamekwenda mbali zaidi na kukusanya nguvu na kujenga jengo la maabara za masomo ya Sayansi, jengo lililogharimu Sh.milioni 45 ambapo wananchi wamechangia Sh.100,000 kwa kila familia na kwamba jengo lipo hatua za umaliziaji.
Papmoja na kuishukuru Serikali kupitia TANAPA na mradi wa TASAF kwa kusaidia ujenzi sambamba na kukamilisha usajili, amewashukuru wananchi wa Oldonyowas kwa kuchangia maendeleo ndani ya kata yao, pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo mpaka
kidato cha nne, fursa inayowawezesha watoto wengi kuendelea na shule pindi wanapomaliza elimu ya msingi.

Sehemu ya picha ikionesha Vyumba viwili vya madarasa na ofisi ndogo ya walimu, jengo linalojengwa na wananchi kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Taifa - TANAPA.
Picha ikionesha wanafunzi wa shule ya Oldonyowas wakiwa darasani
Hivyo makala WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI
yaani makala yote WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wananchiserikali-waondoa-changamoto.html
0 Response to "WANANCHI,SERIKALI WAONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI WA SEKONDARI KUTEMBEA UMBALI MREFU KATA YA OLDONYOWASI"
Post a Comment