TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA

TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA
kiungo : TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA

soma pia


TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na wakala wa forodha katika mpaka wa Horohoro na bandari ya Tanga  juu ya utaratibu na mifumo ya ukaguzi wa bidhaa mbalimbali kabla hazijaingia nchini " Pre- shipment Verification of Conformity (PVoC)", ukaguzi wa bidhaa baada ya kuwasili nchini "Destination Inspection (DI)", uthibitishaji wa bidhaa na matakwa ya viwango.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi za Bandari na  washiriki 33 walihudhuria. Semina hii ilifunguliwa na Thobias Mwilapwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, ambaye alisisitiza washiriki kusikiliza kwa makini taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuepuka gharama ya kupoteza muda na pesa, kwa kutokufuata taratibu au kuingiza bidhaa zilizochini ya kiwango.
 
Baadhi ya washiriki wakati wa majadiliano, waliomba TBS kuhakikisha majibu ya sampuli yanatoka kwa haraka ili kuepuka gharama za ziada ya kuhifadhi mizigo yao. Kwa upande wake Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza washiriki kuwa na hulka ya kutuma malalamiko yao rasmi kwenye dawati la huduma kwa mteja, kupitia namba ya bure ambayo ni 0800110827, ili yaweza kushughulikiwa kuliko kubaki nayo na kusubiri mikutano au semina.

TBS imeendelea kutoa semina kama hizi kwa waagizaji bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha mkoani Mwanza na Dar es Salaam, na hivi karibuni itatolewa pia katika mkoa wa Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa akifungua Semina kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha katika Bandari ya Tanga na Horohoro, katika ukumbi wa Bandari , Machi 20, 2019. Kushoto ni Bw. Cunbert Kapilima, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu(TBS) na kulia ni   Bw. Faustine January, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TBS).
Afisa viwango mwandamizi (TBS), Stephen Rwabunywenge akiwasilisha mada ya matakwa ya msingi wa viwango kwa waagizaji wa mizigo na mawakala wa forodha  katika bandari ya Tanga na Horohoro.
Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Emmanuel Kiwango akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa kufuatwa kwa mizigo inayoingizwa bila kukaguliwa inapotoka na kukaguliwa nchini " Destination Inspection" kwa waagizaji na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na Horohoro.
 Waagizaji mizigo na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na mpaka wa Hororo, wakiwa pamoja na watoa mada wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi.
 Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bi. Janeth Kakuru akiwasilisha mada ya ukaguzi wa bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja hapa nchini (PVoC),kwa waagizaji na mawakala wa forodha mkoani Tanga


Hivyo makala TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA

yaani makala yote TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/tbs-yatoa-semina-kwa-waagizaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA"

Post a Comment