Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa

Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa
kiungo : Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa

soma pia


Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa

Wataalam katika sekta ya maji wanaohuduhuria Kongamano la Kisayansi Kuhusu Sekta ya Maji nchini wametakiwa kutoa elimu kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji ambayo haiongezeki ilhali mahitaji yake yanaongezeka kila siku. 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo jijini Dodoma wakati akiongea na Wataalam na washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili ikiwa ni moja ya matukio ya Wiki ya Maji kitaifa kwa mwaka 2019. 

Prof. Mkumbo amesema miongoni mwa miji inayokua kwa kasi hivi sasa ipo Barani Afrika na kama hatua hazichukuliwa mapema uhaba wa maji utaikumbuka baadhi ya miji ifikapo mwaka 2050. Amesema ni vizuri wataalam wakatumia elimu yao kuwashirikisha wananchi na kutoa elimisha zaidi kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji. 

Prof. Mkumbo amesema ni vizuri kujenga utamaduni wa kuwa na jukwaa la kuwashirikisha watu wengine kuhusu uzoefu na utaalam pamoja na utafiti katika sekta ya maji ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utendaji kazi, na kuhudumia wananchi vizuri zaidi. 

Kufuatia wazo hilo, wataalam na washiriki wa Kongamano la Kisayansi wameazimia kuanzisha chapisho la kitaalam, Jarida la Sekta ya Maji, na kumpitisha Prof. Tolly Mbwete kuwa Mhariri Mkuu mwanzilishi, na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo kuwa mlezi wa jarida hilo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 


Hivyo makala Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa

yaani makala yote Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/jarida-la-kitaalam-kuhusu-sekta-ya-maji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa"

Post a Comment