title : MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE
kiungo : MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE
MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama amewaagiza watendaji wa vijiji na kata, kuhakikisha watoto wa wafugaji walio na umri wa kwenda shule, wanakwenda ili wapate haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wa jamii nyingine.
Aidha ameeleza, wilaya inatarajia kuchukua sensa ya watoto wa wafugaji ili kupata idadi kamili ya watoto hao ambao hawaendi shule hadi sasa.
Assumpter alitoa agizo hilo, wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wafugaji na wakulima, kijiji cha Kwala, Kibaha Vijijini.
Aliwataka ,wafugaji kuacha kuwatumikisha watoto wao kuchunga mifugo hasa ng'ombe badala ya kuwapeleka shule kupata elimu.
"Watendaji nendeni mkahakikishe hakuna mtoto wa mfugaji anaefuga, hawa ndio Sokoine wa kesho, kwenye maziwa kuna akili, wanarubuniwa tuu, ila wafugaji watie akilini kwamba mtoto akizaliwa sio wako ni mali ya serikali "
"Haiwezekani wewe unaenjoy, mnakaa kujiolea wanawake 30, wakati watoto wako hawaendi shule, baadae hawa hawajui kama wataweza kuoa wake wengi hivyo kutokana na uchumi na maisha yanavyobadilika ""alisema Assumpter.
Mkuu huyo wa wilaya alielezea, serikali inajitahidi kujenga mazingira bora ya kielimu na kusomesha watoto bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne lakini jamii hiyo haijatambua umuhimu wa fursa hiyo.
Pamoja na hayo,Assumpter aliwaomba waendelee kuheshimiana ,kuishi kwa upendo kati ya jamii ya wafugaji na wakulima .
Nae makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Esta Moreto aliiasa jamii hiyo kujenga utamaduni wa kusomesha watoto wao badala ya kuwageuza wachungaji wa mifugo ya familia, bali wafanye shughuli hiyo baada ya kutoka masomoni.
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama
Hivyo makala MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE
yaani makala yote MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mshama-awacharukia-wafugaji-wasiopeleka.html
0 Response to "MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE"
Post a Comment