title : WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI
kiungo : WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI
WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI
WAFANYABIASHARA watano wa jijini Dar ea Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manne ya kuingiza kemikali bila kuwa na kibali cha Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Wankyo Simon amewataja wfanyabiashara hao kuwa ni Jumanne Mazunde, Godfrey Kiwelu, Nsia Mbonika, Chanikan Mhina na Joseph Omoll.
Wakisomewa mashtaka yao leo Februari 26.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, imedaiwa, Septemba 13, 2017 huko katika maeneo ya Ubungo Maziwa Dar es Salaam, mshtakiwa Mazunde aliingiza kemikali mbalimbali zenye uzito wa kilogramu 1,514.5 kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia.
Pia mashitakiwa, Godfrey na Mbonika wanadaiwa Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo Dar es Salaam, waliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 87, zilizoingizwa kutoka Nairobi nchini Kenya bila kibali cha mkemia. Imeendela kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo mshtakiwa, Mhina aliingiza kemikali zenye uzito wa kilogramu 100 bila kuwa na kibali cha mkemia.
Katika shitaka la nne, Septemba 13, 2017 maeneo ya Ubungo washtakiwa wote waliingiza kemikali bila kuwa na kibali. Hata hivyo, washitakiwa wamekana mashitaka hayo na kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Akiwasomea msharti ya dhamana, Hakimu Shaidi amewataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini na vitambulisho watakaosaini kulipa Sh milioni 10. Hata hivyo, washitakiwa watatu walipata dhamana huku wawili walirudishwa rumande kwa kukosa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
Hivyo makala WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI
yaani makala yote WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/watano-kizimbani-kwa-kuingiza-kemikali.html
0 Response to "WATANO KIZIMBANI KWA KUINGIZA KEMIKALI NCHINI"
Post a Comment