title : Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi
kiungo : Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi
Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi kutokana na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kudhibiti bidhaa hizo.
Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula leo wakati akifungua mafunzo ya siku Tano kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) pamoja na nchi ya Malawi.
Dkt.Chaula amesema serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa ajili ya kudhibiti dawa ,vipodozi,vifaa tiba ,Chakula pamoja vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Amesema mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo.Amesema kuwa usambazaji wa dawa katika soko umeendelea na viwango ya ubora na salama mpaka katika hatua ya usajili.
Dkt.Chaula amesema serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa ajili ya kudhibiti dawa ,vipodozi,vifaa tiba ,Chakula pamoja vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Amesema TFDA iko nafasi ya tatu katika udhibiti wa dawa na kufanya ni mamlaka ambayo imekuwa na mfumo wa udhibiti wa dawa hadi inamfikia mlaji. “WHO imetutambua na imetupa level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa, hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya kimataifa". Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi".
“Ili tuweze kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”.
Akiwasilisha mada Dkt. Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu.
“Tunayo malengo 17 ya kidunia (SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt. Khademu.
Amesema TFDA iko nafasi ya tatu katika udhibiti wa dawa na kufanya ni mamlaka ambayo imekuwa na mfumo wa udhibiti wa dawa hadi inamfikia mlaji.Nae Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo.
Amesema kuna mwanya wa utekelezaji baadhi ya changamoto katika nchi zinazoendelea katika masuala ya usambazaji wa dawa.Dkt.Shirima amesema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uwezo wa kufanya vizuri na kufanya wananchi wapate huduma bora ya dawa katika usambazaji
Amesema kuwa TFDA inasajili bidhaa za dawa na kuangalia masoko ikiwa ni pamoja kulinda mipaka kwa dawa ambazo hajachunguzwa na Maabara kwa kuhakikisha haziingii katika soko.
Viongozi wakisikiliza maada za wataalam katika mkutano wadau wa udhibiti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Dkt Candida Shirima akizungumza katika mkutano wa wataalam wa udhibiti uliofanyika jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya wataalam wa udhibiti na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
Dkt.Alireza Broojerd wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akizungumza katika warsha wataalam wa udhibiti wa ubora wa dawa na Chakula kutoka Mamlaka za TFDA,ZFDA na Zambia ukifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wataalam wa udhibiti uliofanyika jijini Dar es salaam.
Hivyo makala Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi
yaani makala yote Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tanzania-moja-ya-nchi-yenye-mifumo.html
0 Response to "Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi"
Post a Comment