title : POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI
kiungo : POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI
POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na kumpongeza kwa kazi nzuri kwa kuunganisha wananchi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lugola ambaye utembea na Ilani ya CCM katika mazingira tofauti ikiwemo ofisini na pamoja na mikutano yake ya kikazi, kitendo hicho kinamfurahisha kiongozi huyo wa CCM na kumtaka achape kazi zaidi.
Polepole alikutana na Lugola Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo wakati Waziri huyo alipokua anatoka katika kikao chake na Kamati ya Siasa ya Mkoa ya Chama hicho, alipofanya ziara katika ofisi hizo.
“Mheshimiwa Waziri nakupongeza kwa kuunganisha wananchi na ilani ya CCM, endelea kuchapa kazi,” alisema Polepole. Hata hivyo, Waziri Lugola alimshukuru Polepole kwa kumpa pongezi hiyo na kuahidi kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt John Magufuli katika uongozi wake.
Waziri Lugola yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha, leo. Waziri Lugola alikutana na Polepole mara baada ya kumaliza Kikao chake na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa ambapo Waziri huyo ufanya hivyo kila anapofanya ziara zake mikoani, Polepole alimpongeza Waziri huyo kwa kuunganisha Wananchi na Ilani ya CCM, alitaka azidi kuchapa kazi. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Hivyo makala POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI
yaani makala yote POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/polepole-ampongeza-waziri-lugola-kwa.html
0 Response to "POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUUNGANISHA WANANCHI NA ILANI YA CCM, AMTAKA ACHAPE KAZI ZAIDI"
Post a Comment