WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI

WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI
kiungo : WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI

soma pia


WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma 

WANAFUNZI 346 wa kidato cha kwanza katika Wilaya Kakonko mkoani Kigoma ambao walikuwa hawajaanza masomo kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa madarasa wanatarajia kuanza masomo mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Hatua hiyo inatokana na jitihada za Serikali wilayani humo kuhakikisha wanafunzi waliofaulu na kutakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanakwenda shuleni.

Akizungumza hivi karibuni Ofisa elimu kwa Shule za Sekondari wilaani hapa Christopha Bukombe amesema miongoni mwa wanafunzi 1,714 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza walishindwa kuripoti ni 346 waliopangiwa katika shule ya Kanyonza, Muhange na Gwanumpu.
Bukombe ametoa takwimu hizo baada ya kupokea msaada wa mifuko ya saruji na mabati 60 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa vitano na baada ya mwezi huu kuisha wanafunzi watajiunga kutokana na changamoto kutatuliwa.

Amesema katika shule ya Kanyonza kuna wanafunzi 78, Muhange 97 na Gwanumpu 171 ambapo kutokana na upungufu huo walianza kuhamasisha wananchi kuchangia na Serikali imetoa Sh.milioni 8 katika shule mbili za Kanyonza na Gwanumpu na Sh.milioni 4 kwa shule ya Muhange.

Mchango huo wa umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa lengo la kutatua changamoto hiyo na wanafunzi wataanza masomo kwani walichokuwa wanasubiri fedha kutoka Serikalini.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi saruji na mabati hayo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za wananchi ambazo wamezionesha.

Amewapongeza watendaji wa kijiji, madiwani na wenyeviti wa vijiji kwa jitihada zao kubwa katika kufanikisha ujenzi wa madarasa ili wanafunzi wapate elimu.Amesema Serikali inatamani kuona kila mtoto anapata elimu na ni jukumu la wazazi kujitoa ili kutatua baadhi ya changamoto zinazo jitokeza, kwani Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
"Niwaombe wananchi mnapoambiwa elimu bila malipo si kwamba hata kujitolea kwenye ujenzi mshindwe, watoto ni wa kwenu lazima mnapoona Serikali haijakamilisha jambo fulani mfanye wenyewe suala hili ni letu sote.

"Lazima wanafunzi wote wapate elimu ni haki yao hakuna urithi mwingine tutakao waachia watoto wetu zaidi ya elimu lazima mtambue kuna michango mingine Wananchi wanatakiwa kuchangia kuhakikisha changamoto hizi zinakwisha,"amesema Kanali Ndagala.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Gwanumpu, Toy Butono amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutoa msaada huo na kuwaomba wananchi kuendelea kuchangia.


Hivyo makala WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI

yaani makala yote WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wanafunzi-346-wa-kidato-cha-kwanza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI"

Post a Comment