title : MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI
kiungo : MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI
MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akipokea Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi ya Mtoto kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akikabidhi Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi kwa Afisa Maendeleo ya Jamii aliyewakilisha Mkoa wa Shinyanga wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Katavi wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uelimishaji Jamii kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto wakiwa katika kazi ya vikundi kujadiliana namna bora ya kuwasiligsha mafunzo hayo kwa Jamii kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo mapema leo Katika mji mdogo wa Kasulu.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa ustawi wa Jamii wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Simon Anange amesikitishwa na watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na ndugu na watu walioaminiwa kuwalea au kuwatunza iwe nje au manyumbani kwao.
Akifunga Mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu matumizi ya Kitini cha Malezi ya Mtoto na Familia yalitolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendelep ya Jamii Kanali Anange amesema amesema asilimia 40 ya vitendo vya ukatili inafanyika mashuleni ikiwemo utani wa kumdhalilisha mtu na kufanya watoto kuichukia shule.
Akiutaja unaofanyika mashuleni Kanali Anange amesema ni ukatili wa kunyanyasa mtu kwa kumtania jambo ambalo limechangia baadhi ya watoto wanaokumbwa na kadhia hiyo kugoma kwenda shule.
Aidha Mkuu wa Wilaya hiyo amelitaja tatizo la kibinafsi kuwa linachangiwa na wazazi wa siku hizi kuwalea watoto katika mazingira ya kujitenga tofauti na hapo awali ambapo mtoto kimsingi alikuwa ni mtoto wa Jamii nzima.
Amesema tatizo tulilonalo la watoto wa mitaani linatokana na malezi mabaya kwani katika Jamii ya watu wa Zanzibar hakuna watoto wa mitaani akiitaja Tanzania bara kukosa upendo kwani Jamii yetu inayojiita imeendelea imezidisha ubinafsi kwa kuwa na upendo tu kwa watoto walio wazaa tu bila kuangalia watoto wengine walipokosa upendo na kukimbilia mitaani.
Ameitaja jamii kuanagalia kile tunachokiita kuendelea kama kinaleta tija kwani maendeleo ya sasa ya mtoto kula katika saani peke yake kinamfanya kufikili kuwa cha kwake ni cha kwake matokeo yake ni kuwa na jamii yenye ubinafsi na maendeleo ya sasa yanakiuka misingi muhimu kama zamani kwa kisingizio cha maendeleo na kuongeza kuwa wakati mwingine maendeleo ya sasa yanaipeleka jamii kuendekeza mambo yasiyokuwa ya razima.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amesema ili kuweza kuendeleza Jamii zetu Serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto imejipanga kutokomeza mila mbaya katika Jamii na kuenzi mila nzuri lakini pia kuitaka jamii kutambua kuwa kuna tofauti kati ya kutunza na kulea watoto.
Aidha Bi. Mwangwa amesema kuwa Serikali imejiwekea malengo kupitia mpango kazi huo kuwa ifikapo mwaka 2022 serikali iwe imetokomeza vitendo vya ukatili katika Jamii na kuongeza kuwa mpango huu pia unaangalia mazingira salama ya mtoto akiwa shuleni lakini pia katika Jamii.
Mafunzo haya kuhusiana na malezi ya mtoto na familia yamefanyika kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Kigoma na Katavi na mikoa hii kwa kiasi kikubwa ina changamoto ya uwapo wa mimba na ndoa za utotoni lakini yanafanyika huku Taifa likuwa linakumbwa na kitisho kipya cha mauaji ya watoto.
Hivyo makala MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI
yaani makala yote MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mkuu-wa-wilaya-asikitishwa-na-watu-wa.html
0 Response to "MKUU WA WILAYA ASIKITISHWA NA WATU WA KARIBU NA WATOTO KUWA CHANZO CHA UKATILI"
Post a Comment