Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi

Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi
kiungo : Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi

soma pia


Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi

Na Grace Semfuko-MAELEZO 

Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa kushirikiana na Magnet Youth Sports Organization ya Tanzania February 15 hadi 19 mwaka huu walishirikiana katika kuandaa safari ya kitalii ya kocha andreas Pach na Martin Hammel wa Ujerumani ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea vivutio vya Utalii lengo likiwa ni kuutangaza Utalii wa Tanzania. 

Andreas Pach na Mwenzake Martin Hammel ni Makocha ambao wapo nchini Tanzania wakitokea kwenye mradi wa ITK Pathfinder 2019 uliopo chini ya Chuo Kikuu cha Leipzig cha nchini Ujerumani mradi ambao unalenga kuwafundisha Makocha na Vijana kwenye mchezo wa Soka na kumtangaza Mchezaji nyota mwenye asili ya Tanzania anaechezea Ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani Yusuph Poulsen. 

Wakiwa Nchini Tanzania Makocha hao walipata nafasi ya kutoa mafunzo ya michezo kwa makocha 25 na Vijana 120 wa Kitanzania lengo likiwa ni kukuza Vipaji vya michezo nchini. 

Ujio wa makocha hao ni mwaliko wa Magnet Youth Sports Organization chini ya Mkurugenzi mwendeshaji wake Tuntufye Mwambusi ambapo bodi ya utalii kupitia ujio huo wameamua kushirikiana katika kuutangaza utalii wa ndani ikiwepo Mlima Kilimanjaro 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema bodi hiyo imeanza mazungumzo ya wali na mchezaji huyo nyota Yusuph Poulsen ambaye anachezea ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani ili kuutangaza Utalii wa ndani. 

“kwetu sisi TTB tunachukulia ujio huu wa makocha hawa na mashirikiano yaliyopo kati ya ITK na Tanzania, na tumeanza mazungumzo na Mchezaji mwenye asili ya Tanzania Bw. Yusuph Poulsen ikiwa ni mkakati wetu wa kutumia watu maarufu katika kuutangaza utalii wa ndani na tunataka kumfanya kuwa Balozi wa hiyari wa utalii wa Nchi yetu” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. 

Nae mmoja kati ya makocha hao wawili wa kutoka Nchini Ujerumani Bw.Andreas Pach alisema Tanzania kuna Vipaji vingi vya Michezo na hivyo ni muhimu kuviendeleza. 

“tumefurahishwa kuona Watanzania ni watu wakarimu, Tanzania kuna Vijapi vingi vya Michezo na vipaji hivi vikiendelezwa tutakuwa mbali kimichezo, Poulsen anafanya Vizuri sana kule Ujerumani” alisema Andreas Pach 

Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji wa Magnet Youth Sports Organization Bw. Tuntufye Mwambusi alisema wataendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na wanamichezo katika kukuza Utalii wa Tanzania.


Hivyo makala Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi

yaani makala yote Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mchezaji-wa-ujerumani-mwenye-asili-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Kuutangaza Utalii wa Tanzania nje ya Nchi"

Post a Comment