title : Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020
kiungo : Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020
Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akizungumza Katika ziara yake ya kukagua miradi ya elimu ya SEKONDARI mwingine Mwenyekiti wa mtaa wa Bonyokwa Kisiwani Peter Mwasingi (PICHA NA HERI SHABAN)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akitoka kukagua majengo ya sekondari ya Pugu Nyamwezi katika Zara endelevu kukagua ujenzi wa SEKONDARI Picha na Heri Shaban
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri akichanganya udongo katika miradi ya shule za sekondari katika ziara yake endelevu Picha na Heri Shaban
Na Heri Shaban
MANISPAA ya Ilala katika bajeti yake ya Mwaka wa fedha 2019/2020 inatarajia kutenga shilingi bilioni 8 sekta ya elimu ili iweze kuondokana na changamoto ya vyumba vya Madarasa katika Manispaa hiyo.
Hayo yalisemwa Dar es salaam na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri wakati wa ziara endelevu ya kukagua miradi ya Shule za Manispaa hiyo .
"Ili kuondokana na changamoto ya vyumba vya madarasa na madawati katika Manispaa hii bajeti ijayo nitatenga bilioni 8 zote ziweze kuelekeza katika sekta ya elimu " alisema Shauri.
Shauri alisema bajeti ya mwakani ya elimu tayari imeshatengwa hivyo katika Manispaa Ilala watakuwa na vyumba vya madarasa ya kutosha ujenzi wake unatarajia kuanza Mwaka huu mpaka hapo watakuwa wametekeleza agizo la Rais wa awamu ya tano John Magufuli Mpango wa elimu bure.
Alisema Elimu ndio ulithi pekee utakao dumu kwa watoto wetu katika Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli kama Ilala tukalazimika kutenga bilioni 3 ambayo imefanikisha kujenga vyumba 127 vya wanafunzi ili wale waliokosa waweze kusoma.
Aidha Shauri alielezea mafanikio sekta ya elimu Msingi Mwaka huu Ilala kitaifa imeshika nafasi ya nne Kati ya shule 185.
Aliwataka Watendaji, Wenyeviti wote wa Manispaa ya Ilala kufanya kazi kwa kufuata sheria sambamba kuangalia miradi ya elimu iliyopo katika kata zao na kuangalia thamani ya ubora iendane na fedha .
Aliwagiza Wakandarasi wote wanaojenga madarasa mpaka kufikia February 25 wawe wamemaliza ujenzi huo.
Kwa Upande wake Ofisa Elimu Sekondari Manisipaa Ilala Elzabeth Ngonyani alisema katika manispaa hiyo mpaka kufikia mwisho wa Mwezi January Mwaka huu wanafunzi 6000 wa kidato cha kwanza walikuwa bado kuripoti shule kuanza masomo lakini mpaka sasa wamefanikiwa wamepatikana wanafunzi 3000.
"Awali katika ziara ya Mkuu ya Ilala Sophia Mjema kulikuwa na upungufu wa wanafunzi wa kidato cha kwanza tukaweka mkakati tumefanikiwa kupata wanafunzi 3000 Kati ya 6000 wanafunzi wengi Wapo shule binafsi
Mwisho
Hivyo makala Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020
yaani makala yote Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/manispaa-ya-ilala-yatenga-bilioni-8.html
0 Response to "Manispaa ya Ilala yatenga bilioni 8 sekta ya elimu 2019/2020"
Post a Comment