title : MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA
kiungo : MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA
MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA
Na Munir Shemweta, BUCHOSA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa hati za ardhi kwa wananchi kumi na tisa wa halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza na kuifagilia halmashauri hiyo kwa kuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za majalada ya ardhi.
Dkt Mabula alitoa pongezi hizo leo tarehe 15 Februari 2019 alipozungumza na wananchi wa Buchosa wakati wa kukabidhi hati za ardhi akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli yaserikali kupitia kodi ya ardhi.
Alisema,kwa mara ya kwanza katika ziara zake kwenye halmashauri mbalimbali ameikuta halmashauri ya Buchosa ikiwa inatunza kumbukumbu za majalada ya ardhi kwa mujibu wa sheria sambamba kuwepo mawasiliano kati ya afisa mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kushughulikia majalada na kuongeza kuwa migogoro mingi ya ardhi inayojitokeza inasababishwa na utunzaji mbaya wa majalada ya ardhi.
"Taratibu za utunzaji majalada ya ardhi pamoja na mawasiliano baina ya ofisa mmoja na mwingine zimekaa vizuri ni tofauti kabisa na niliyoyaona katika halmashauri nyingine, Buchosa mko vizuri" alisema Dkt Mabula.
Alizungumzia utoaji hati kwa wananchi wa Buchosa, Dkt Mabula aliwapongeza wananchi hao kwa kupatiwa hati na kueleza kuwa wananchi hao wanaelewa kuwa ardhi ni mali na hati walizokabidhiwa zitawawezesha kukuwa kiuchumi.
Alisema, mambo makubwa yanayofanyika nchini kama ununuzi wa ndege, mradi wa treni ya mwendokasi, mradi wa kufufua umeme wa Stiglers George ni jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwahudumia wananchi na hayo yote yatafanikiwa kwa wananchi kutekeleza jukumu la kulipa kodi ikiwemo ile ya ardhi.
Aliongeza kwa kusema wananchi 19 waliopewa hati watafungua milango kwa wananchi wa Buchosa na wengine kuchangamkia kupata hati ambapo pengine walikuwa hawajui kama hati inaweza kupatikana Buchosa na kuongeza kuwa wale wananchi walio katika urasimishaji nao wachangamkie kupata hati.
Hata hivyo, Dkt Mabula pamoja na kuipongeza halmahauri ya Buchosa lakini ameilaumu kwa kushindwa kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji na kuiagiza halmashauri hiyo kuanza kupanga na kupima pamoja na kuanisha maeneo ya huduma.
Awali,Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Buchosa Rafael Kilumanga alisema halmashauri hiyo imepima jumla ya viwanja 886 katika maeneo tofauti ya halmashauri hiyo na viwanja 31 kati ya vilivyopimwa 31 vimemishamilikishwa kwa wananchi na kutolewa hati.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimpatia hati ya kumiliki ardhi mkazi wa Buchosa mkoani Mwanza Esta Bukombe wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya ardhi. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akikagua mafaili katika masijala ya ardhi ya Halmashauri ya Buchosa, kushoto ni Afisa Ardhi Mteule Rafael Kilumanga. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)
Hivyo makala MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA
yaani makala yote MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mabula-akabidhi-hati-za-ardhi-na-kuipa.html
0 Response to "MABULA AKABIDHI HATI ZA ARDHI NA KUIPA TANO HALMASHAURI YA BUCHOSA"
Post a Comment