AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE

AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE
kiungo : AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE

soma pia


AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE

Awilo Longomba ni majina maarufu miongoni mwa wapenzi wa muziki wa dansi sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki na Kati. Unaweza kumfananisha kwa kiasi fulani na mwanamuziki Bileku Mpasi kufuatia historia zao katika muziki kushabihiana. Wakati Awilo alianza kupata umaarufu akiwa akicharaza drums katika bendi mbalimbali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bileku alikuwa maarufu kwa ‘kurap’ pia umahiri wa kunengua katika bendi ya Empire Bakuba, chini ya Kabasele Yampanya ‘Pepe Kalle’

Hivi sasa wanamuziki hao wanamiliki bendi zao. Muziki wake umekuwa wa Kimataifa baada ya kulishirikisha wanamuziki wengine wakimataifa likiwemo kudi la PSqure toka nchini Nigeria. Awilo amekuwa kivutio kikubwa katika maonesho takriban yote kufuatia uwezo wake wa kuimba na kunengua pia uchangamfu wake jukwaani.

Wengi tumezoea kumuita Awilo Longomba, lakini majina yake halisi aliyopewa na wazazi wake baada ya kuzaliwa ni Albert William Longomba. Baba yake mzee Vicky Longomba alikuwa akitokea katika mkoa wa Mongo na mama yake Mkoa wa Ngombe huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Awilo anatalanta za kupiga drums, kutunga na kuimba nyimbo, aliyepata fursa ya kufanya kazi katika bendi kadhaa nchini humo zikiwemo za Stukas Mombombo Kayima, iliyokuwa ikiongozwa na Lita Bembo, Viva la Musica ya marehemu Papa Wemba, Loketo group iliyokuwa ikiongozwa na Aurlus Mabele, Nouvelle Generation pamoja na Bongo Wende.

Bendi yake ya mwisho kwake kuitumikia ilikuwa ya La Nouvelle Generation. Mnamo mwaka 1995 Awilo aliamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea ‘Solo artist’. Ili kuonesha kuwa yeye ni mkali katika muziki, alitoa albamu yake ya kwanza ya ‘Moto Pamba’ mwaka huohuo akiwa amejiongeza yeye mwenyewe kutunga na kuimba nyimbo zote pamoja na kupiga drums.

Albamu hiyo aliifyatua baada ya kupata msaada kutoka baadhi ya wanamuziki wakubwa akina Shimita El Diego, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko, Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star. Awilo katika albamu hiyo iliyopokelewa vilivyo na mashabiki wake, ilimtambulisha mkali huyo hadi kupelekea kupata mialiko lukuki ndani na nje ya nchi yake.

Albamu hiyo ya ‘Moto Pamba’ ilimpa tuzo ya kwanza ya kuwa mwanamuziki bora Afrika ya Kati zilizoandaliwa na Kora Music Awards zilizofanyika katika jiji la Sun City nchini Afrika ya Kusini mwaka 1996.

Mwaka 1998 alithibitisha kuwa hatanii, aliingia tena studio ambako alirekodi albamu yake ya pili iliyopewa majina ya Coupe Bibamba ikiwa na maudhui ya kuelezea hali ya umasikini katika nchi za Kiafrika.

Kwenye albamu hiyo baadhi ya nyimbo alimshrikisha mwanadada kutoka kundi la Cassav aitwae Jocelyne Berourd. Coupe Bibamba iliweza kumsafishia njia Awillo Longomba kupata mafanikio na ndoto zake kuzidi kutimia. Baadhi ya mafanikio yake yalidhihirika mnamo mwaka 2001 alipopata tena tuzo nyingine ya Kora Music Awards iliyoitwa ‘Judges Special Award’ kupitia albamu yake ya tatu Kafou Kafou.

Awillo mwenye machachari jukwaani, alitoka tena na albamu ya ‘Mondongo’ aliyoifyatua mwaka 2004. Katika albamu hiyo alifanikiwa kuwashirikisha  wanamuziki wengine wenye majina makubwa katika muziki nchini DRC, akina Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky Kiambukuta na Simaro Lutumba.

Awilo ni mwanamuziki anayejituma vilivyo katika kuandaa kazi za muziki hali iliyopelekea kupata mialiko mingi katika nchi nyingi Barani Afrika.
Baadhi ya nchi hizo ni Tanzania, Mali, Togo, Benin, Ivory Coast, Kenya, Burkina Faso, Nigeria na Cameroon. Aidha Awilo alivuka mipaka ya Bara la Afrika hadi nchi za Barani Ulaya zikiwemo za Uingereza, Ubelgiji, Switzerland, Ufaransa pamoja na bara la Amerika ikiwemo Canada.

Huko aliambatana na kundi la kitamaduni la kimataifa la kusakata au kucheza ngoma (Nabtry International Cultural Dancers). Kundi hilo lilikuwa la Kiafrika lililokuwa likicheza ngoma lililoanzishwa mwaka wa 2007 na Grace Haukwa. Ubunifu wake wa kurudia upya wimbo wa ‘Maze’ wa Tabu Ley Rochereau, alifanikiwa ‘kuwakamata’ wapenzi na mashabiki wake.

Kama Wahenga walivyotangulia kusema kuwa “Mtoto wa nyoka ni nyoka”. Awilo anatoka katika familia ya wanamuziki ikizingatia kwamba baba yake Victor Longomba ‘Vicky’, alikuwa katika sekta ya muziki akiwa mwanachama mwanzilishi wa bendi iliyokuwa kubwa nchini humo ya Tout Puissant OK. Jazz (TP OK. Jazz)  ya Franco Luanzo Makiadi.

Katika bendi hiyo Vicky Longomba alikuwa ni mwimbaji kiongozi wa bendi hiyo.Familia ya mzee Vicky Longomba ilikuwa ni ya wanamuziki zaidi. Ikumbukwe kuwa hata kaka yake Lovy Longomba ambaye ni marehemu, alitamba sana wakati akiwa katika bendi za Super Mazembe na Shika Shika katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Baadaye Lovy Longomba akahamia nchini Tanzania ambapo alijiunga katika bendi ya African Sound Orchestra (Afriso Ngoma).Pia Lovy alikuwa baba wa familia yenye watoto wanamuziki akiwamo binti yake aliyerithi uimbaji aliyejulika kwa majina ya Elly Longomba.

Aidha alikuwa na watoto mapacha Christian na Lovy, ambao wote ni nyota katika muziki wa Hip-hop, wakimiliki Kampuni ya ‘Longambas’ ambalo ni maarufu la Afro-Fusion lenye makao katika jiji la Nairobi nchini Kenya.Maisha ya nguli Lovy Longomba yalikatishwa ghafla katika ajali ya gari iliyosababisha kifo chake katika ardhi ya Tanzania mwaka 1996.

Siri kubwa ya mafanikio ya Awilo Longomba katika muziki ni kitendo cha kushirikiana na wanamuziki wengine wakubwa. Mfano aliungana kupiga muziki na wanamuziki kama Kanda Bongoman, Oliver Ngoma, Tshala Muana na hata kundi la PSquare la nchini Nigeria.

Mnamo 2008 Awilo Longomba alitoa albamu mpya ya Super-Man, ambayo ilikuwa fanikio lingine kubwa. Kutokana na kura za umaarufu na ushindi wa kihistoria katika Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu huku nchi zaidi ya 120 zikipiga kura, albamu mpya ya Awilo, Super-Man, ilishinda tuzo la mtumbuizaji bora wa Soukous wa mwaka 2009.

Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Nabtry Grace Haukwa ambaye anamwakilisha Awilo nchini USA alikuwepo kupokea tuzo hilo kwa niaba ya Awilo katika sherehe ya Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu.

Awilo Longomba kwa sasa anaishi katika jiji la Paris nchini Ufaransa, akiwa na uhusiano wa karibu wa kimapenzi na mwanamuziki Barbara Kanam. Hivi karibuni Awilo ameachia wimbo mpya wa ‘Bundelele’,ambapo ameonekana kuwa karibu na wasanii wakubwa wa Nigeria. Lakini picha iliyowekwa na Peter Okoyo wa P-Square inaashiria neema zaidi kwa Longomba aliyepo nchini Nigeria kujitangaza zaidi


Hivyo makala AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE

yaani makala yote AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/awilo-longomba-toka-kuongozwa-hadi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE"

Post a Comment