Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp

Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp
kiungo : Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp

soma pia


Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp

*Lengo ni kujua changamoto zao, kuzitatua haraka

Na Said Mwishehe-Blog ya Jamii-Arusha

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka mfumo maalumu wa kutumia magurupu ya WhatsApp (Jukwaa), kwa lengo la kutoa na pokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wao wa kada mbalimbali nchini.

Akizungumza na leo jijini Arusha Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, amesema kuanzishwa kwa magroup ya WhatsApp lengo ni kutoa taarifa kwa wateja wao nchini kote umetokana na maagizo ya bodi ya shirika hilo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

“Tunatambua nguvu ya magurupu ya WhatsApp katika kufikisha taarifa kwa jamii, hivyo TANESCO tumeona hili na hivyo kupitia Bodi yakatoka maagizo maalumu kwa wilaya zote na mikoa nchini kuwahakikisha yanaanzishwa magurupu hayo.

“Hivyo mameneja wa TANESCO kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa yato nchini wameanzisha magurupu hayo kwa ajili ya kuwasiliana na wateja. Kupitia magurupu mbali ya kuwa na wateja wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wa TANESCO na lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati ili wateja wetu wajue,” amesema Muhaji.

Amesema tangu kuanzishwa kwa magurupu hayo kumeleta faida kubwa kwani hivi sasa wateja wa shirika hilo wanao uhakika wa kupata taarifa ya kila kinachoendelea na wakati huo huo wateja nao wanayo fursa ya kuwalisha changamoto iwapo zitajitokeza.

Ameongeza katika kuhakikisha magurupu hayo yanaleta tija zaidi kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa walichokifanya ni kuweka magurupu kulina na aina ya wateja, hivyo yapo magurupu kwa ajili ya wateja wakubwa ambapo miongoni mwao wamo wawekezaji.

“Kuna magurupu ya wateja wa kati na magurupu ya wateja wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.“Tuliamua pia kwenye magurupu hayo wamo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya mtaa, wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine wa Serikali ambao ni sehemu ya wadau muhimu katika kuhakikisha tunatatua changamoto za umeme.

“Kwa maana hiyo hata Mkurugenzi Mtendaji wa shirika letu katika mtaa anaoishi ameunganishwa kama mteja wa TANESCO kwenye grupu la WhatsApp na wakati huo kama kiongozi,” amesema

Alisema kupitia mfumo huo wamepata faraja kuona yamekuwa msaada mkubwa wa kufikisha taarifa zao kwa wateja huku akisisitiza kwa sasa wanahimiza wilaya zote za TANESCO kuhakikisha wanaanzisha magrupu hayo kwa wale ambao bado.

Amesema kwa Dar es Salaam kupitia magurupu hayo wamekuwa wakipata taarifa kutoka wa wateja wao kwa haraka zaidi na watendaji wa Shirika wanatafuta ufumbuzi kwa haraka.Ukweli njia hii ya mawasiliano imekuwa na tija kubwa kwetu na tutaendelea kuitumia.

Leila ambaye yupo kwenye ziara ya wahariri wa vyombo vya habari mkoani Arusha yenye lengo la kuangalia miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano amesisitiza umuhimu wa magurupu hayo ambapo wawekezaji wa mkoa huo wamekiri kuwa sasa imekuwa rahisi kwao kupata taarifa mara kwa mara.

Wakizungumza na Blog ya Jamii baadhi ya wamiliki wa viwanda waliopo mkoani Arusha , wamesema kwa sasa wanajiona wenye thamani kutokana na namna ambavyo TANESCO imeamua kuwaweka karibu kupitia njia hiyo ya kuwasiliana.


Hivyo makala Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp

yaani makala yote Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tanesco-yaunga-wateja-wake-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tanesco yaunga wateja wake kwenye WhatsApp"

Post a Comment