title : ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA
kiungo : ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA
ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Hamis Ulega ametoa mafuta ya diesel Lita 1000 kwa ajili ya greda ambalo husaidia kutatua changamoto za barabara jimboni humo pamoja na shuka 100 kwa kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyika wilayani humo, Ulega amesema kuwa ameamua kutoa mafuta changamoto iliyotokana na Halmashauri kununua greda muda mrefu lakini limekaa bila kufanya kazi.
"Nilitoa msukumo kwa kukaa pamoja na madiwani na kushauriana kwa pamoja tuwe na greda letu wenyewe ili itusaidie kutatua changamoto za barabara hasa za vijijini ambako barabara nyingi hazipitiki na tumenunua greda hilo kwa zaidi ya milioni 700 ikiwa ni fedha zetu wenyewe na likachonge barabara zetu." Amesema Ulega.
Ulega amesema kuwa greda hilo alikodishwi kwa wananchi ila kinachotakiwa vijiji vijichangishe wanunue mafuta kwa shughuli za kutatua kero za barabara. "Sio kwamba nimeshindwa kutoa hela Mkurugenzi hela nakukabidhi mapipa haya matano ya mafuta kila moja lina Lita 200 yakatumike ipasavyo."Amesema Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi shuka 100 Mkurungenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde zenye thamani zaidi ya milioni moja.kushoto ni Mganga Mkuu wa wa wilaya ya
Mkuranga, Dkt.Stephen Mwandembo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akimsikiliza Mzee Athuman Mtalu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mkuranga mko wa Pwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wananchi katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyikawa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Baadhi ya wananchi wakimsiki Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA
yaani makala yote ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ulega-afunga-mwaka-kwa-kutatua.html
0 Response to "ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA"
Post a Comment