title : TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI
kiungo : TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI
TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI
Na Emanuel Madafa, Mbeya
Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema wao kama shirikisho la vyama vya vya wafanyakazi hawana ugomvi na Rais Magufuli na kwamba ujio wake Mkoani Mbeya katika sherehe Mei Mosi kuna uwezekano wa kutamkwa jambo kubwa ambalo litaleta faraja kwa wafanyakazi Nchini.
Nyamhokya ametoa kauli hiyo jijini Mbeya katika kikao cha maandalizi ya sherehe za wafanyakazi nchini ambapo kitaifa itafanyika mkoani huku mgeni rasmi anatatajiwa kuwa Rais Magufuli.
“Sisi kama TUCTA hatujawahi kuwa na ugomvi na Rais Magufuli , yapo mambo madogomadogo ambayo kwa upande wetu tumekwosha yaweka sawa “Amesema Nyamhokya.
Amesema yapo Mambo mengi ambayo amewachia wafanyakazi likiwemo suala la kikotoo hivyo kwa ujio wake mkoani Mbeya katika sherehe hizo kuna uwezakano mkubwa akatoa majibu ya maswali ambayo wafanyakazi wengi wamekuwa wakijiuliza.
“Maadhimisho haya yanafanyika Mbeya lakini nchi nzima macho na nasikia yatakuwa hapa wanamuangalia huyu ni Rais wetu “Amesema Tumaini Nyamhokya .
Sherehe hizo za siku ya wafanyakazi Mei Mosi zinatarajiwa kufanya mkoani Mbeya ambapo mgeni rasmi anatajwa kuwa Rais Dkt Magufuli.
Katika hatua nyingine Rais hiyo wa TUCTA amesema wananchi wa mkoa wa Mbeya wajiandae kwa ajili ya kupokea ugeni huu kwani anaamini yapo mambo mengi ambayo yatanufaisha Mkoa huu .

Rais wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini, Tumaini Nyamhokya akizungumza katika kikao cha kwanza kwa ajili ya maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi ambapo Kitaifa zitafanyika Mkoani Mbeya huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt Magufuli.


Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Mei Mosi wakimsikiliza kwa makini Rais wa TUCTA (hayupo pichani) Tumaini Nyamhokya katika kikao cha kwanza cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi zitakazo fanyika mkoani Mbeya ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt Magufuli.
Hivyo makala TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI
yaani makala yote TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/tucta-hatuna-ugomvi-na-rais-magufili.html
0 Response to "TUCTA HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI"
Post a Comment