UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA
kiungo : UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

soma pia


UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

WAKATI Tamasha la Pasaka likijiandaa kuwasha moto katika Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka  Alex Msama ametoa mwito kwa wasanii mbalimbali nchini wakiwamo wa muziki wa Injili kuhakikisha wanafuata na kuheshimu Sheria za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Msama amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia msimu mpya wa Tamasha la Pasaka ambalo linatarajia kuanza Aprili 21,2019.Amefafanua tamasha hilo litaanzia Katika Jiji la Dar es Salaam na kauli mbiu ya tamasha hilo inasema Umoja na upendo huduma amani ya nchi yetu.

Kuhusu wasanii kufuata Sheria za BASATA, Msama ametoa mwito kwa wasanii kuiheshimu Baraza hilo na kwamba wasanii ambao watashiriki ni wale ambao wamejisajili na kutambuliwa kisheria.

Kuhusu tamasha hilo amesema BASATA tayari wametoa  maelekezo yenye lengo kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa. "Siku zote usipokuwa na msimamizi huwezi kufanya vizuri, Wasanii wengi wanakuwa na dharau, bila BASATA tamasha hili lingekuwa limekufa siku nyingi", amesema Msama

Katika hatua nyingine, Msama amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na wasanii kutoka mataifa ya nje, kuhakikisha nao wanapata mualiko ili  washiriki tamasha hilo.

"Wasanii wote ambao watashiriki ni wale wanaoiheshimu BASATA, ni vema wasanii wakahakikisha wanafuata sheria katika kufanya kazi zao za sanaa", amesema Msama .Msama muda si mrefu wataanza kutaja majina ya wasanii ambao watashiri tamasha hilo na kueleza kwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika pia katika Jiji la Dodoma.

Wakati huo huo Msama amesema katika kipindi cha tamasha la Pasaka watatumia pia nafasi hiyo kuendelea kumuombea Rais  Dk.John Magufuli, Makamu wa  Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Tamasha la Pasaka jijini Dar es salaam,ambalo linatarajiwa kuanza kurindima Aprili 21,2019.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Alex Msama akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka,mbele ya waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam,kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo Jimmy Charles.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu maendeleo ya maandalizi ya tamasha na ujumbe muhimu kwa wasanii/waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo.


Hivyo makala UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA

yaani makala yote UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/ujumbe-wa-alex-msama-kwa-wasanii.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UJUMBE WA ALEX MSAMA KWA WASANII KUELEKEA KUANZA KWA TAMASHA LA PASAKA"

Post a Comment