Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu

Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu
kiungo : Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu

soma pia


Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu

Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa Filamu Wastara Issa ili aweze kwenda kupatiwa matibabu India ya mguu wake unaomsumbua.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu nyumbani kwake jana Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu wake uliyokatwa mpaka kufikia kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.

“Ndugu zangu watanzania najua kutoa ni moyo na siyo utajiri ninawaomba mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani mpaka sasa anahitaji kiasi cha milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha safari yake hiyo ya kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye matibabu hayo mwezi ujao,”Dkt.Mwakyembe.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa wito kwa wasanii wote wa filamu nchi kujitokeza na kumsadia mwanatansia mwenzao wa filamu katika kufanikisha anapata matibabu ili aweze kurudi na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .

“Bodi ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa laTaifa tumetoa kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya kumchangia katika kufanikisha safari yake ya matibabu na serikali kwa ujumla inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha msanii huyu anapata kiasi hicho cha pesa kilichobakia,”Bibi Fissoo.

Pamoja na hayo Katibu Mtendaji BASATA Bw.Godfrey Mngereza alitoa wito kwa wasanii wote nchini kwa nao kijitokeza kumchangia msanii huyo kwani wasanii wote ni wamoja kwa maana wote ni wanafanya kazi ya sanaa hivyo ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.

Kwa upande wa msanii Wastara Issa aliishukuru serikali kwa kumtembelea na kumjulia hali pamoja na kumchangia na kusema imekuwa nifaraja kubwa kwake kuwaona na alitoa akaunti namba anayotumia kwa ajili ya kukusanyanyia michango ambayo ni EQUITY BENKI – 3007111415583 na namba za simu anazotumia kuchangisha ni 0768 – 666 113 na 0713 666 113 na alieleza amesajiliwa kwa jina la Wastara Issa katika namba hizo za simu pamoja na akaunti namba yake.


Hivyo makala Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu

yaani makala yote Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/watanzania-tumsaidie-msanii-wastara.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Watanzania Tumsaidie Msanii Wastara Kuweza Kupata Matibabu"

Post a Comment