title : SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?
kiungo : SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?
SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
INGAWA Ulimwenguni kuna madaraja mengi makubwa na ya kila aina ila kuna madaraja yanatambuliwa kuwa ya kushangaza zaidi. Kwenye Nchi ya Uingereza kuna madaraja kadhaa ya kuogofya ikiwemo daraja la Queen Elizabeth II ambalo linaunganisha pia nchi Scotland na Wales.
Kumekuwa na maoni kwamba baadhi ya madaraja yamekuwa ni ya kuogofya kwa maumbo na miundo yake, Mfano tu, Mamlaka nchini Italia imeagiza ukaguzi wa madaraja yote baada daraja la Morandi kubomoka na kupelekea vifo vya watu 43 mwezi wa nane mwaka jana.
Mtandao wa ClickMechanic umefanya utafiti na kutoa orodha ya madaraja ya kushangaza, kuogofya na ambayo huwapa ugumu zaidi madereva kuendesha vyombo vya usafiri na madaraja hayo ni pamoja na:
1. Daraja la Eshima Ohashi nchini Japan
Daraja hili lina urefu wa mita 1,700 na limejengwa katika urefu wa kwenda juu (kutoka usawa wa bahari) karibu mita 45 na hivyo kuwezesha meli kubwa kupita chini. Mwinuko wa Daraja hilo ni wa kushangaza na kustaajabisha upatapo nafasi kulitembelea. Daraja la Eshima Ohashi linaunganisha majiji ya Matsue na Sakaiminato huku mwinuko wake wa karibu asilimia 6.1 inafanya ujihisi unapandisha mlima hivi. Pamoja na kuwa na urefu(kwa umbali) wa mita 1,700 na kimo cha urefu kwenda juu karibu mita 45 hakulifanyi kuwa daraja kubwa zaidi ingawa linaruhusu Meli kupita chini yake.
2. Daraja la Storseisundet nchini Norway,
Daraja hili lina muonekano wa kushangaza kutokana na upepo na mawimbi makubwa toka baharini huleta ugumu kwa madereva kuendesha. Unapokuwa upande wa kulia, unaweza kuhisi daraja hilo halijakamilika au muundo wake umeishia karibu tu. Inawezekana ndio daraja ambalo picha zake zimetumika zaidi. Daraja hili linaunganisha peninsula ya Romsdal na kisiwa cha Averøya kilichopo kwenye Bahari ndogo ya Norway. Muundo wake wa nusu duara wenye umbali wa mita 260 za urefu huweza kukufanya ufikiri daraja halijakamilika katika upande wake wa pili.
3. Daraja la Millau Creissels nchini Ufaransa
Hili ni daraja refu kwenda juu zaidi ulimwenguni kwa kimo cha mita zipatazo 343. Wakati mwingine madereva na vyombo vya usafiri hujikuta wakipita kwenye mawingu wanapokatiza kwenye daraja hilo kutokana na urefu wake. Lilichora na mbunifu kutoka Uingereza Lord Norman Foster na mchoro kufanyiwa kazi na Mhandisi mfaransa Michel Virlogeux. Mwaka 2006 Daraja hilo lilishinda Tuzo ya Muundo bora duniani kutoka kwenye Chama cha Kimataifa cha Madaraja na Wahandisi Miundo kuonesha jinsi gani limeshinda yote kwa Ubunifu uliotumika.
4. Daraja la Hong Kong–Zhuhai–Macau nchini China.
Ni daraja refu zaidi ulimwenguni linalokatiza Baharini, kwa kuwa na umbali unaofikia maili 34 huku likiunganisha majiji matatu liyopo kwenye Mto Pearl Delta. Daraja hili limekamilika mwaka jana na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Daraja la Jiaozhou lenye urefu wa maili 26 pia la nchini China.
Daraja la Hong Kong–Zhuhai–Macau ni muunganiko wa madaraja matatu, njia ya chini ya bahari na likiunganisha visiwa vinne ambavyo ni vya kujengwa. Ujenzi wake umetumia nadharia na muundo kama wa daraja la Chesapeake kwenye ufukwe wa Virginia. Kuna Vibali 10,000 vya magari vimetolewa kupita katika daraja hili kutoka Hong Kong kwenda Zhuhai. Haitoshi, magari yanayoingia jiji la Hong Kong na Macau kutoka sehemu nyingine hupaswi kulipia vibali vya kila siku.
5. Daraja la Nanpu nchini China.
Daraja lenye viunga na mipishano kama chakula cha tambi ni maarufu duniani kote. Daraja la Nanpu lipo Shanghai linadhihirisha mchanyato wa ubunifu na uhandisi uliotamalaki. Mzunguko na kunesa kwa daraja huweza kumfanya dereva kupata kizunguzungu wakati wa kupita katika daraja hili. Nanpu limejengwa kwa namna ya kupunguza matumizi makubwa ya ardhi hivyo basi ni daraja mzunguko wa kuvutia na kustaajabisha.
Hivyo makala SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?
yaani makala yote SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi? mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/shauku-na-kuogofya-haya-ndio-madaraja.html
0 Response to "SHAUKU NA KUOGOFYA: Haya ndio madaraja ya kushangaza zaidi?"
Post a Comment