title : IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA
kiungo : IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA
IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA
NA VERO IGNATUS-ARUSHA.
Kutokana na wingi wa wakinamama wenye tatizo la ugonjwa wa fistula kuendelea kujitokeza na kupata matibabu katika kituo maalumu cha Kivulini Maternity Center kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha,imeelezwa kuwa kwasasa idadi ya wagonjwa wa tatizo hilo imepungua kwa kiasi kikubwa mkoani humo
Akieleza ukubwa wa tatizo hilo daktari Francis Mollel ambae ni mtaalamu wa magonjwa wakina mama anasema kuwa kutokana na elimu ya masuala ya afya ya uzazi kumesaidia kupunguza idadi ya wagojwa wa fistula kwani husababishwa na uzazi pingamizi.
Namba ya wagonjwa inaendelea kupungua kutokana na elimu ya afya imekuwa ikitolewa mara kwa mara, uelewa ni mkubwa kwa wagonjwa kwenda hospitali mapema kujifungua kwani tatizo hili la fistula linatokana na uzazi pingamizi. ''Alisema Dkt Mollel
Dkt. Mollel amesema kuwa wagonjwa wa mwisho waliofanyiwa upasuaji walikuwa 23, na hivi karibuni wanatarajia upasuaji mwingine kufanyika machi 2019 idadi itaongezeka zaidi kwani wanatazamia kuingia kwenye kambi za wakimbizi pia
Katika hatua nyengine mtaalamu huyo amebainisha namna wanavyo wanawafikia na kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na tatizo la fistula hususani katika maeneo ya vijijini ambapo amesema kambi ya fistula wanaifanya kila baada ya miezi mitatu.
Mara nyingi tunawatuma wataalamu wetu kwenda kuwatafuta wagonjwa huko nje, ambapo wakishapimwa na kugundulika kuwa wana fistula yenyewe, tunawalaza, tunawafanyia upasuaji, mgonjwa anakaa hospitalini siku 14 na tunamuangalia kama hana tatizo tena tunamruhusu kurudi nyumbani akiwa ameshapona kabisa. '' Alisema Dkt.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho gambo ambae ametembelea kituo hicho kwa lengo la kufahamu maendeleo na changamoto za utioaji huduma kwa wagonjwa akatumia fursa hiyo kuahidi kufanyia changamoto zilizo katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na changamoto ya hitaji la damu salama pamoja na barabara kufika eneo la kituo.
''Changamoto kubwa ya waliyonayo chanjo, damu salama na wametuomba kama mkoa kuwasaidia, pia wana changamoto ya barabara hivyo tumezungunza na Tarura kama wanaweza kutengeneza barabara ya kilometa 1.2''Alisema Gambo
Mratibu wa TARURA Mhandisi Edward Amboka akiahidi kuanza kufanya tafiti kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo mara moja.
Kituo hicho ni maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye tatizo la Fistula na uzazi hususani wagojwa walio masikini bila gharama yoyote.
Dkt. Francis Mollel ambae ni Mtaalamu wa Magonjwa ya wakina mama. Picha na Vero Ignatus.
Hivyo makala IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA
yaani makala yote IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/idadi-ya-wagonjwa-wa-fistula-yapungua_9.html
0 Response to "IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA"
Post a Comment