title : WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA
kiungo : WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA
WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA
Na Veronica Simba – Chato
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewasha umeme katika Kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita, tukio lililoibua shangwe na nderemo kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika jana, Desemba 21, 2018 kijijini hapo, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na kuzungumza na wananchi.
Akizungumza na wananchi, Waziri Kalemani aliwataka wautumie umeme huo katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuendeshea viwanda vidogovidogo vya kusaga na kukoboa nafaka, kuchomelea vyuma na vingine vya aina hiyo. “Umeme huu siyo kwa ajili ya kuwasha taa tu. Ni umeme unaotosha kwa matumizi ya viwanda, hivyo basi utumieni ipasavyo ili kuboresha maisha yenu,” alisisitiza Waziri.
Aidha, aliwahamasisha wananchi ambao hawajalipia, waendelee kulipia ili waunganishiwe huduma hiyo muhimu. Halikadhalika, aliwashauri wananchi wenye matumizi madogo ya umeme, kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ili kuondokana na gharama za kufunga nyaya katika nyumba zao.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi Desemba 21, mwaka huu ambapo pia aliwasha rasmi umeme kijijini hapo.
Wananchi wa kijiji cha Iparamasa wilayani Chato, wakiwa wamejipanga kumpokea na kumsalimia Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), alipowasili kuzungumza nao na kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 21 mwaka huu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), akijumuika kucheza na wananchi wa kijiji cha Iparamasa wilayani Chato, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 21, mwaka huu.
Mzee Yohana Masanyiwa akisoma risala kwa niaba ya wazee wa kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato; kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 21, mwaka huu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA
yaani makala yote WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-kalemani-aibua-shangwe-iparamasa.html
0 Response to "WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA"
Post a Comment