title : WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA
kiungo : WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA
WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda amewataka wananchi kuudhuria maonyesho ya Viwanda yanayofanyika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Kakunda amewataka wananchi na wadau mbalimbali wajitokeza na kushuhudia maonyesho hayo ili waweze kujionea mambo mbalimbali yalioandaliwa na wenye viwanda.
Alieleza maonyesho ya mwaka huu lengo lake kubwa ni kuhamasisha watanzania kujenga viwanda.
“Katika maonyesho haya wadau wa sekta ya Viwanda watajadiliana na kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini”.
Mhe.Waziri alisema maonyesho ya mwaka huu yataunganisha wenye viwanda, wazalishaji wa malighafi mbalimbali na huduma nyingine zinazotumika viwandani, watafiti na wabunifu ili kujadilaiana na wenye viwanda umuhimu wa kuboresha teknologia za uzalishaji na Tehama katika viwanda ili kutoa fursa kwa wananchi kufahamu fursa zilizopo na kuweongezea hamasa zaidi ili kuwekeza katika kwenye ujenzi uchumi wa Viwanda.
“Changamoto za wekezaji zitatatuliwa kupoitia cliniki ya Biashara itakayotoa huduma mbalimbali ndani ya uwanja ikiwemo usalama mahali pa kazi, taratibu za kupata maeneo ya uwekezaji, mitaji, leseni ,ubora wa bidhaa teknologia ya viwanda vidogo na , kutumia vipimo, kusajili biashara kwa njia ya mtandao kuyatambua masoko ya nje na ndani ya nchi.”
Maonesho ya Viwanda yameshirikisha waoneshaji 513 kutoka sekta ya Viwanda vikubwa,vya kati na vidogo vilevile taasisi za fedha na Serikakali.
Hivyo makala WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA
yaani makala yote WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-awakaribisha-wananchi-kujionea.html
0 Response to "WAZIRI AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIONEA MAONYESHO YA WIKI VIWANDA"
Post a Comment