DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO

DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO
kiungo : DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO

soma pia


DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ameiomba mahakama kutoa huduma ya sheria kwa wananchi kizalendo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Sheria wilayani humo jana katika uwanja wa Taifa mjini Namtumbo Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wanasheria kutenda haki katika kuzingatia uzalendo katika nchi yao.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo alidai yapo malalamiko machache kuhusu kukilalamikia chombo hicho cha mahakama katika ofisi yake hali inayoonesha sehemu kubwa ya chombo hicho kinatenda haki alisema mkuu wa wilaya huyo.

Hata hivyo aliwataka wananchi wilayani hapa kukitumia chombo hicho cha mahakama kuwafikisha wahalifu wanaoweka mimba wanafunzi badala ya wazazi kuendesha mashauri ya mimba majumbani na kumaliziana kinyumbani huku wanafunzi wa kike wakikosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Namtumbo Bi. Gloria Lwomile alimwambia Mkuu wa wilaya changamoto ya kucheleweshwa kwa upelelezi kutoka jeshi la polisi husababisha kesi nyingi kuchukua muda mrefu pamoja na changamoto ya uchache wa watumishi wa mahakama wilayani humo.

Lwomile alidai mahitaji ya watumishi wilayani humo ni mahakimu 2 katika mahakama ya mwanzo na aliopo ni mmoja na pia katika mahakama ya wilaya mahitaji ya mahakimu ni watumishi 9 na waliopo ni watumishi 7.

Iddi Chowo mkazi wa Namtumbo alisema maadhimisho ya siku ya sheria yameweza kumwongezea ufahamu hasa katika swala la kumwekea mtu dhamana haihitajiki kutoa fedha bali kinachohitajika ni kukamilisha taratibu za kumwekea mtu dhamana alisema bwana chowo.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria wilayani Namtumbo yalifanyika katika kiwanja cha Taifa mjini Namtumbo ambapo awali yalitanguliwa na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu kufahamu mambo ya sheria.

 Picha ya kwanza inaonesha Mkuu wa wilaya Namtumbo akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya sheria wilayani Namtumbo ambapo waliaswa kutumia taaluma zao kutenda haki kwa wananchi.



Hivyo makala DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO

yaani makala yote DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dc-namtumbo-aiomba-mahakama-kutoa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO"

Post a Comment