UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE
kiungo : UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

soma pia


UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

*Mkurugenzi Mtendaji Mkuu atangaza uhakiki wa wafanyakazi nchi nzima
*Azungumzia kuanza kufanya tafiti kubaini wasomaji,wasikilizaji wa vyombo vyao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Faustine Sungura ameamua kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao.

Amesema motisha hiyo inakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wote na hasa katika kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018.

Akizungumza leo ofisini kwake Sungura amesema Desemba 28 mwaka huu wa 2018 amekutana na wafanyakazi wote kwa kada mbalimbali na alitumia sehemu hiyo kuelezea mikakati ya kampuni hiyo ambayo imedhamiria kufanya mambo makubwa.
 
"Tulipokutana na wafanyakazi kuna mambo mengi ambayo tumeyazungumza.Pia nilitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya. Rais wetu amefanya mambo makubwa kwa mwaka huu yakiwamo ya kuboresha sekta ya anga, miundombinu kwa upanuzi wa barabara na ujenzi wa madaraja, umeme wa mto Rufiji ,ununuzi wa korosho, elimu bure na mambo mengine mengi ambayo yamefanyika.Hivyo wafanyakazi hawa wamekuwa wakiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais,"amefafanua.

Ameongeza wafanyakazi wa Uhuru Media Group kwa mwaka huu wa 2018 wamefanya kazi kwa bidii, hivyo ameamua kuwapongeza kwa kuwapa motisha kwani kesho ni Januari moja ni vema wakauanza mwaka vizuri."Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na wasioajiriwa lakini wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vya chama tutawapa motisha hiyo.Tutafanya kwa walioko Dar es Salaam na wa mikoani," amesisitiza.

Aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini."Nataka kumuona kila mfanyakazi uso kwa uso .Rais wetu aliamua kufanya uhakiki kwa watumishi wa Serikali ,nami namuunga mkono kwa kufanya uhakiki wa wafanyakazi wetu."amesema Sungura.
 MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Faustine Sungura akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao,aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini na kuchukua hatua.
 MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura  akielezea mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake jijini Dar,namna kampuni  hiyo inavyojipanga ,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini."Pia Februari mwaka 2019 tutafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyetu na Aprili 2019 tutafanya uzinduzi rasmi,ambapo ndio tutazungumza malengo na mikakati yetu.",alifafanua Sungura.
  MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi kutoka Idara ya Utawala,Banga Lucas kiasi cha fedha ikiwa ni sehemu ya motisha iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa  kampuni hiyo ikiwa kama sehemu ya kuthamini mchango wao.Picha na Michuzi Jr-MMG.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Hivyo makala UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

yaani makala yote UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/uhuru-media-group-yawapa-motisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE"

Post a Comment