title : TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA
kiungo : TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA
TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA
KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.
Vijana kutoka Chuo Cha Munister nchini Ujerumani, leo wametembelea Kituo cha Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo Kigamboni Dar es Salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira.
Vijana hao zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani na baadaye kushiriki katika mafunzo ya ushonaji nguo kwenye mradi wa ushonaji nguo wa kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazokabili vijana na kinamama.
Kituo hicho cha Taasisi ya TaDEDO hadi sasa kina vijana 83 ambao kwa namna mojawapo walikosa fursa ikiwemo ya kutoendelea na masomo ambao sasa wanapatiwa mafunzo ya ujasiriamali wa kubuni na kushona nguo ambapo baadhi yao tayari ni mafundi.
Vijana wa Kituo cha ubunivu na ushonaji nguo cha Taasisi ya Kijamii ya TaGEDO, wakimwelekeza jinsi ya kutumia cherehani, kijana Astrid Naundorf kutoka Chuo Kikuu Cha Munister, wakati vijana wa Chuo hicho walipotembelea Kituo hicho, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
Taasisi ya Kijamii ya kuelendeleza Vijana na Kinamama katika Ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) Venance Kalumanga akichoma taka, wakati yeye na wenzake wa Taasisi hiyo, walipoungana na Vijana kutoka Chuo Cha Munister nchini Ujerumani, kufanya usafi kwenye eneo la Ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni, dar es Salaam, leo
Vijana wa TaGEDO wakishirikiana na Vijana hao kutoka Ujerumani kukusanya taka wakati wakifanya usafi kwenye ofisi ya Mtaa wa Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam, leo.
Hivyo makala TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA
yaani makala yote TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/tagedo-yapata-ugeni-kutoka-ujerumani.html
0 Response to "TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI, WAFANYA SHUGHULI MBALIMBALI IKIWEMO USAFI WA MAZINGIRA"
Post a Comment