title : Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana
kiungo : Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana
Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana
Majid Abdulkarim
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango wote wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao katika kukuza uchimi wanchi ili kuleta matokeo bora kwa watanzania wanao watumikia.
Hayo yamebainishwa leo wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 yatakayo fanyika leo na kesho hapa jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. Dk. Chaula amesema mafunzo hayo ni fursa kwa maafisa hao kuhakikisha wanapata ujuzi wa kuweza kupata matokeo bora katika kukuza uchumi wanchi hii.
“Ili kufikia matokeo bora ya kukuza uchumi wa nchi hii mnatakiwa kuwa wabunifu kwa kuchukua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ili kuinua uchumi nchi hii” Alisema Dk. Chaula.
Dk. Chaula ameongeza kuwa kila mtumishi wa Umma anadhamana kubwa kwa taifa hili , na dhamana yenyewe ni kuhakikisha tunawatumikia vyema watanzania wenzetu ili kuleta matokeo bora kwa nchi yetu kama Muhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyo fanya mpaka leo kupitia matokeo yake tunamkumbuka. Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango OR-TAMISEMI, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo maafisa hao watanufaika kwa kupata uelewa wa kuandaa bajeti iliyobora na kuwa walimu wazuri kwa maafisa wengine katika maeneo yao ya kazi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.
Baadhi ya Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango wa Halmashauri nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula (hayupo pichani) leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana
yaani makala yote Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ufunguzi-wa-mafunzo-ya-maandalizi-ya.html
0 Response to "Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana"
Post a Comment