SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA
kiungo : SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

soma pia


SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuenzi misingi ya utawala bora haitamvumilia kiongozi yeyote wa umma atakayekiuka misingi hiyo na kutanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma katika utendaji wake.

Amesema mgongano wa maslahi umechangia rasilimali za nchi kunufaisha watu wachache huku wananchi wengi kuendelea kuwa fukara, wakati wachache wakijitajirisha isivyo halali, hivyo Serikali itaendelea kuziba mianya, kwani ikiachiwa iendelee, itarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mmomonyoko wa maadili umechangia sana kutozingatiwa kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma, tatizo ambalo limesababisha mgongano wa maslahi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 10) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma, ambapo ametumia Napenda fursa hiyo kuwaasa viongozi wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao kwani hiyo ndio njia pekee itakayoepusha mgongano wa maslahi.

Waziri Mkuu amesema mgongano wa maslahi ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kuisababishia hasara Serikali kwa muda mrefu, tatizo ambalo lazima lidhibitiwe kwani mara kadhaa baadhi ya viongozi au watumishi wa umma wamekuwa wakifanya maamuzi kwa mambo wanayojua wazi kuwa wana maslahi binafsi nayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Desemba 10, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchil Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavinde na kulia ni  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Profesa, Faustine  Kamuzora. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

yaani makala yote SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/serikali-haitomvumilia-kiongozi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA"

Post a Comment