title : SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO
kiungo : SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO
SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO
NTEGHENJWA HOSSEAH – TAMISEMI, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jaffo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara hii lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI .
Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”.
Aliongeza kuwa nahitaji “Consistency of information” kutoka kwa watalaam wanaofahamu vizuri maeneo yao ya kazi sio kila siku unahamisha unaanza na mtu mpya naye anakuwa hana taarifa za kutosha kuhusu kazi za awali hivyo inachukua muda kuanza kwenda sawa kwangu mimi nasema ntamnyoosha yeyote ambaye haendani na viwango vyangu akiwa hapa hapa na si kwingineko”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapopichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda
Hivyo makala SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO
yaani makala yote SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/sitahamisha-mtumishi-nitatengeneza.html
0 Response to "SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO"
Post a Comment